ULIPITWA NA HII:LIST YA WAUZA MADAWA YA KULEVYA ALIYOKABIDHIWA RAIS MAGUFULI
Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na
mijadala lukuki kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na biashara haramu
ya madawa ya kulevya. Wapo wanaharakati na wanasiasa kadha wa kadha
wamekuwa wakifanya jitihada za kutaka kutaja majina ya walio nyuma ya
biashara hii, lakini mwishoni hupatwa na kigugumizi na kuishia hewani.
Marehemu Amina Chifupa (MB), aling'aka
bungeni na kutangaza kwamba anayo majina ya wanaojihusisha na biashara
hii haramu na atayataja muda wowote, lakini kwa bahati mbaya
akatangulia mbele ya haki kabla ya kutimiza azma yake hiyo.
Rais mstaafu wa awamu ya nne ya JMT,
Mhe. Jakaya Kikwete alinukuliwa akisema amepatiwa majina ya watu wazito
wanaojihusisha na biashara hiyo, lakini naye mpaka anaondoka
madarakani, hakuchukua hatua zozote.
Yupo Blogger Mtanzania aishiye
ughaibuni anayeitwa Mange Kimambi, naye amekuwa mstari wa mbele kupiga
kelele kuhusu vigogo wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya
inayoangamiza vijana wengi na kuharibu nguvukazi ya taifa, lakini mpk
sasa Jeshi la Polisi na vyombo vya usalama nchini vinaonekana kusua sua
kulivalia njuga suala hili.
Leo, gazeti la Jamhuri limeandika
orodha ya majina ya wanaohusishwa na biashara hii ya madawa ya kulevya
ambayo yamekabidhiwa kwa waziri wa mambo ya ndani, Mhe. Charles
Kitwanga ambaye ameyafikisha kwa Mheshimiwa John Pombe Magufuli (kwa
mujibu wa gazeti hilo).
Je, hii inatoa ishara njema ya 'kutumbuliwa jipu' hili la muda mrefu?
Sources; DJ SEK BLOG
0 comments: