YAWEZEKANA NA YAKO IPO:Nywila zilizotumiwa sana na watu 2015
Kampuni ya usalama mtandaoni ya SplashData imetoa orodha ya nywila au maneno ya siri yaliyotumiwa sana na watu mwaka uliopita.
Orodha hiyo imetayarishwa kwa kutumia maneno ya siri zaidi ya milioni mbili yaliyofichuliwa na wadukuzi mwaka uliopita.
Mwaka huu, neno ‘Star Wars’, kutoka kwa mwendelezo wa filamu za Star Wars, lilikuwa miongoni mwa maneno 25 yaliyotumiwa zaidi. Filamu ya Star Wars: The Force Awakens ilizinduliwa mwezi Desemba.
Wengi bado wanatumia ‘123456’ kama nywila na wengine ‘password’.
Ili kuwa salama mtandaoni, huwa ni vyema kutumia nyila ambayo watu wengine hawawezi wakaifikiria au kugundua kwa urahisi.
Moja ya njia za kuimarisha neno la siri ni kuchanganya tarakimu, herufi na alama pamoja na kuchanganya herufi kubwa na ndogo.
Lakini wengi hutatizika katika kukumbuka nywila.
Moja ya njia unazoweza kutumia ni kuangalia maneno ya wimbo uupendao na kuyafupisha.
Hapa, tunakupa mfano wa jinsi unaweza kupata nyila kutoka kwa wimbo.
- Chagua mwanamuziki umpendaye, tuseme kwa mfano Diamond Platinumz.
- Chagua wimbo, kwa mfano Mdogo mdogo
- Tafuta mstari mmoja, sana ukupendezao zaidi, mfano mstari wa kwanza: ‘Nimetembea tembea bara na visiwani’
- Fupisha kwa kuchukua herufi ya kwanza ya kila neon, au herufi mbili za kwanza. Tukichukua herufi mbili za kwanza, tunapata ‘Nitebanavi’
- Changanya herufi kubwa na ndogo, unaweza kupata kwa mfano ‘NiteBANAvi’ kutoka kwa mstari wetu.
- Kisha, badilisha herufi zinazokaribiana na tarakimu kuwa tarakimu, mfano badala ya ‘a’ tumia ‘@’ na badala ya ‘i’ tumia ‘1’.
Katika mfano wetu, tutapata ‘N1teB@N@v1’. Ni vigumu mtu kuigundua kwa urahisi lakini kila ukikumbuka wimbo wako unaweza ukaikumbuka kwa urahisi.
Nywila zilizotumiwa sana 2015
1. 123456
2. password
3. 12345678
4. qwerty
5. 12345
6. 123456789
7. football
8. 1234
9. 1234567
10. baseball
11. welcome
12. 1234567890
13. abc123
14. 111111
15. 1qaz2wsx
16. dragon
17. master
18. monkey
19. letmein
20. login
21. princess
22. qwertyuiop
23. solo
24. passw0rd
25. starwars
chanzo:bbcswahili
0 comments: