ASKARI WAFUKUZWA KAZI BAADA YA MFUNGWA KUPATA MIMBA GEREZANI
Askari jela wanne nchini Vietnam
wamesimamishwa kazi kwa kosa la kuzembea kazini baada ya mfungwa wa kike
aliyehukumiwa kunyongwa kushika mimba.
Wachunguzi wanasema Nguyen
Thi Hue, 42, alijitungisha mimba kwa kutumia mbegu za kiume kutoka kwa
mfungwa wa kiume, ili kukwepa hukumu ya kifo.
Sheria ya Vietnam
inasema mwanamke mjamzito au mwenye mtoto wa chini ya umri wa miaka
mitatu hawezi kunyongwa na badala yake hukumu yake inafaa kubadilishwa
na kuwa kifungo cha maisha jela.
Sasa inatarajiwa kwamba hukumu
yake itapunguzwa kutoka kifo hadi maisha jela kwa sababu atakuwa na
mtoto wa chini ya miaka mitatu.
Maafisa wanasema Hue alinunua mbegu kutoka kwa mfungwa wa kiume wa umri wa miaka 27 kwa $2,300 (£1,600).
Mfungwa huyo alimpa mbegu zake mara mbili Agosti mwaka 2015.
Mwanamke huyo anatarajiwa kujifungua Aprili.
Kisa hicho kimetokea katika mkoa wa Quang Ninh, kaskazini mwa nchi hiyo ingawa polisi bado hawajakizungumzia.
Mwaka
2007, askari jela wawili katika mkoa wa Hoa Binh kaskazini mwa nchi
hiyo walimruhusu mwanamke kushika mimba akiwa jela, kwa mujibu wa gazeti
la Thanh Nien. Alikwepa kunyongwa..
chanzo:bbcswahili

0 comments: