KWELI ITAWEZEKANA..?
Tai kuteka ndege zisizokuwa na rubani Uholanzi
Maafisa wa polisi nchini Uholanzi wameanza kuwafunza tai kuteka ndege zisizokuwa na rubani zikiwa angani.
Katika
video moja iliyochapishwa kwenye mtandao tai anaonekana akiitwaa ndege
moja isiyokuwa na rubani kwa makucha yake angani na kupaa nayo.Hii ni baadhi tu ya mbinu zinazojaribiwa na maafisa wa polisi nchini Uholanzi kukabiliana na kuenea kwa matumizi ya ndege zisizokuwa na rubani zinazorushwa angani bila idhini.
Polisi walishirikiana na kampuni moja ya Guard From Above kuwafunza tai hao.
Tai hao wanafunzwa kuteka nyara ndege hizo ziosizokuwa na rubani kwa kudhania kuwa ni mlo.
"Tai hao wanafunzwa kuchukulia ndege hizo zisizokuwa na rubani kama mlo hivi, na hivyo kama kawaida wanaiteka kwa haraka na kuificha mbali'' taarifa hiyo ya polisi inasema.
Ndege hizo zisizokuwa na rubani zimekuwa nyingi sana angani Uholanzi na sasa maafisa wanaosimamia usalama wa ndege nchini humo wanasema zinatishia usalama wa ndege zinazowabeba abiria.
Majuzi tu nusura ndege moja isiyokuwa na rubani isababishe ajali mbaya.
Vilevile kuna hofu kuwa ndege hizo huenda zikatumiwa na magaidi kutekeleza mashambulizi ama hata kupeleleza majengo lengwa.
Vile vile kuna ile hatari kuwa tai hao wanaweza kujeruhiwa na propela za ndege hizo.
Ilikuzuia hilo watawavisha tai haop nguo nzito.
chanzo:bbcswahili
0 comments: