Polisi ajipata 'danguroni' kimakosa
Tembea tembea ya
afisa mmoja wa polisi nchini Uingereza nusura imtumbukize ''pabaya''
alipoingia katika jumba moja la starehe lililokuwa limekodishwa kwa
minajili ya kuandaa sherehe ya wanawake kuadhimisha miaka 50 ya mwenyeji
wao.
Konstabo wa polisi Mike Ober alikuwa katika pita pita yake
katika eneo la Avon Uingereza aliposhangaa kuona mlango klabu moja
maarufu ikiwa wazi.Aliposogelea kupeleleza kunani , alipigwa na butwaa, wanawake walipomshangilia kwa ''huba'' na ''uchu''.
Wengine walimtaka avue nguo mara moja ili ''awatumbuize''
Aliulizwa kama ndiye aliyeagizwa awape burudani ?
Ndipo akang'amua kuwa siye aliyekuwa anatarajiwa ila ni mwanaume wa kukodiwa kuwatumbuiza mabibi waliokuwa wanasheherekea miaka 50 ya mmoja wao ,,,''alilazimika kuondoka mara moja.''
''Mbona umekuja mapema sana?''
''Tupe muda kidogo tujiandae kidogo kisha urejee'' alimweleza bi kizee mmoja.
''Nililazimika kuondoka mara moja'' alisema afande huyo mwenye umri kati ya miaka 20-27.
Alipokuwa akiondoka alikutana na mwanamume mmoja akifululiza kuelekea ndani ya jumba hilo la starehe
chanzo:bbcswahili
0 comments: