KWA HILI MUNGU AINGILIE KATI.
Waanglikana waunga mkono ndoa za jinsia moja
Justin Welby
Waumini wengi wa Kianglikana nchini Uingereza wanaunga mkono ndoa za wapenzi wa jinsia moja ,kulingana na kura ya maoni.
Kati
ya zaidi ya waanglikana 1,500 waliohojiwa asilimia 45 ilisema kuwa ndoa
za wapenzi wa jinsia moja zinafaa kuendelea huku asilimia 37 ikisema
kuwa ni makosa.Kura hiyo ya maamuzi ya Yougov pia imesema kuwa kuna ongezeko la waumini wa kanisa hilo wanaounga ndoa za jinsia moja katika kipindi cha miaka mitatu iliopia.
Miaka mitatu iliopita,kura kama hiyo ya Yougov ilibaini kwamba asilimia 38 ya Waanglikana wanaunga mkono ndoa hizo huku asilimia 47 wakipinga.
Wasiounga mkono wako katika kundi la wanaume walio zaidi na umri wa miaka 55.
Chanzo:bbcswahili

0 comments: