JELA MIAKA 22
Waliomuasi Kagame kufungwa miaka 22 jela
Aliyekuwa mlinzi wa
rais Paul Kagame na mshirika wake wanakabiliwa na hukumu ya miaka 22
gerezani kwa kupanga njama dhidi ya kiongozi huyo wa Rwanda.
Afisi
ya kiongozi wa mashtaka nchini Rwanda imeitaka mahakama iwahukumu
kifungo cha miaka 22 kanali Tom Byabagamba aliyeiongoza kikosi cha
kumlinda rais , na brigedia mstaafu jenerali Frank Rusagara kwa makosa
ya kuchochea uma dhidi ya rais Kagame.Maafisa hao wakuu jeshini walikamatwa mnamo mwezi Agosti 2014.
Wamekanusha madai dhidi yao.
Kiongozi huyo wa Mashtaka alisema mahakamani kuwa Brig-jenerali Rusagara alisikika akiituhumu serikali ya Rwanda kuwa "taifa linalotawaliwa kiimla na kuwa ni taifa lililofeli'
Aidha alidai kuwa '' bwana Kagame ni kiongozi wa kiimla''.
kanali Byabagamba anatuhumiwa kwa kudai kuwa kundi la wapiganaji wa kihutu wa FDLR, waliotekeleza mashambulizi mengi katika taifa jirani la jamhuri ya Congo hawakuwa tishio kwa rwanda.
chanzo:bbcswahili

0 comments: