AUAWA NCHINI SYRIA

...................

Gaidi mwandamizi wa al-Qaeda auawa nchini Syria


Gaidi mwandamizi wa al-Qaeda auawa nchini Syria
Kamanda mwandamizi wa kundi la kigaidi la Ahrar al-Sham lenye mafungamano na mtandao wa kimataifa wa al-Qaeda ameuawa katika hujuma ya bomu iliyolenga ngome za kundi hilo katika mkoa wa Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria.
Majid Hussein al-Sadeq pamoja na magaidi wengine watatu waliuawa katika shambulio la jana Jumamosi dhidi ya mji wa Binnish, unaohesabiwa kuwa moja ya ngome za magaidi hao, yapata kilomita 10 kaskazini mashariki mwa mkoa wa Idlib.
Julai mwaka jana, kamanda mwingine mkuu wa kundi la kigaidi la Ahrar al-Sham kwa jina Abu Abdu Rahman Salqin aliuawa katika shambulio jingine la bomu katika eneo la Abu Talha, mkoani Idlib.
Kwa muda mrefu sasa serikali ya Syria imekuwa ikisisitiza kuwa magaidi nchini humo wanapata misaada ya fedha na silaha kutoka nchi za Magharibi hasa Marekani na waitifaki wake katika eneo hili ambao ni Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na utawala haramu wa Israel. Karibu watu nusu milioni wameshapoteza maisha tokea magaidi waanzishe kampeni ya kumuondoa madarakani Rais Bashar al Assad wa Syria mwaka 2011.
Hii ni katika hali ambayo, Steffan de Mistura, Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria amesema watu wapatao laki nne wamepoteza maisha kutokana na vita vya zaidi ya miaka mitano vilivyoikumba nchi hiyo ya Kiarabu



Chanzo: http://kiswahili.irib.ir/habar
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: