VIDEO: Kondomu inavyotumika kufukuza wanyama Tarangire Arusha
Shirika
la HoneyGuide Arusha kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo jirani na
mbuga ya Tarangire walibuni njia ya kufukuza wanyama ili wasiharibu
mazao yao na kuwafukuza mbali na makazi yao.
Unaambiwa
wamekuwa wakitumia Kondomu kuzuia wanyama kama tembo kuharibu
mazao. Imeelezwa kuwa wanatumia mchanganyiko wa baruti ya pilipili na
kondomu kufukuza wanyama waharibifu. Mchanganyiko huo ukitupwa hewani
Tembo wanapofikiwa na ile harufu ya pilipili ukimbia au kusogea mbali
zaidi.
Njia hii imeelezwa kufanya kazi vizuri na pia imekuwa ikisaidia wanyama kutopata madhara.mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka shirika la HoneyGuide, Ng’orongo Nyamoni Ng’orongo ambaye ameeleza namna wanavyotumia Kondomu kufukuza wanyama………
>>>’Tumetumia
kondomu kama tu kiwezeshaji cha kuweza kubeba mchanganyiko kati ya
mchanga na hiyo pilipili na kwa sababu kondomu inayeyuka haraka na
kulipuka kwa urahisi’
chanzo: http://millardayo.com

0 comments: