HII KALI YA MWAKA ILIYOTOKEA HUKO MAJUU
Atolewa kwenye ndege kwa kuongea Kiarabu
Mwanafunzi wa chuo
kikuu raia wa Iraq katika jimbo la California nchini Marekani anasema
kuwa alitolewa kutoka kwenye ndege ya shirika la ndege la Southwest
baada ya kufanya mazungumzo kwa lugha ya kiarabu.
Shirika hilo la
Southwest lilisema kuwa Khairuldeen Makhzoomi aliondolewa ndegeni tarehe
9 mwezi Aprili kabla ya ndege hiyo kupaa.
Bw Makhzoomi anasema
alikuwa akizungumza na mjomba wake kwa njia ya simu kuhusu hotuba ya
katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Anasema kuwa mwanamke mmoja kwenye ndege hiyo alimkodolea macho wakati alitamka jina "Inshallah" akimaanisha Mungu akipenda.
Baada ya kutumia jina hili mfanyikazi wa shirika la Southwest alimsindikiza nje ya ndege.
Bw
Makhzoomi ambaye aliingia nchini Marekani kama mkimbizi kutoka Iraq na
sasa ni mwanafunzi wa chuo cha Carlifonia cha Berkeley, aliambiwa kuwa
hawezi kuingia tena kwenye ndege hiyo.
chanzo:bbcswahili
0 comments: