WATUMIAJI WA MTANDAO WA YAHOO MNALIFAHAMU HILI....?
Hofu kwa watumiaji wa mtandao wa Yahoo baada ya taarifa za wateja wake milioni 500 kuibiwa
Kampuni
ya mtandao wa Yahoo, inasema kuwa udokozi wa taarifa za wateja wake
zaidi ya milioni 500 duniani, ulikuwa ni mpango uliofadhiliwa na
Serikali, wizi ambao ni mkubwa zaidi kuwahi kufanyika katika historia ya
uharamia wa kimtandao.
Wizi huu
umehusu taarifa binafsi za watu, ikiwemo majina na barua pepe, pamoja
na maswali ya kiusalama ambayo mtu huyatumia kwaajili ya kuthibitisha
akaunti yake.Uharamia huu wa taarifa ulifanyika mwaka 2014 lakini taarifa hizo zimewekwa wazi mwaka huu.
Tayari shirika la ujasusi la nchini Marekani FBI limesema limeanza kuchunguza tukio hili.
Yahoo imesema kuwa “taarifa zilizoibiwa ni pamoja na majina, anuani za barua pepe (emails), namba za simu, tarehe za kuzaliwa, nywila (passwords), lakini sio taarifa za benki,” ilisema taarifa ya Yahoo.
End of break ads in 22s
Publicite, fin dans 22 secondes
Habari za kuwepo kwa tukio la uharamia wa taarifa za kampuni hii ya masuala ya teknolojia, zilianza kuvuma mwezi Agosti mwaka huu, pale maharamia wanaofahamika kwa jina la “Peace” walipokuwa wakijaribu kuuza taarifa za watumiaji milioni 200 wa Yahoo.
Alhamisi ya juma hiki Yahoo ilisema kuwa, taarifa zilizoibiwa ni nyingi kuliko vile walivyokuwa wakibashiri hapo awali.
Nchini Uingereza, kampuni ya ISP Sky na BT wametoa onyo kwa wateja wao kuwa wanaweza kuathirika kutokana na wizi huu, ambapo Yahoo ni mtoa huduma namba moja kwa makampuni hayo, na kuwataka wateja wake wabadili Passwords zao
chanzo: http://sw.rfi.fr/

0 comments: