MAKONDA ASEMA;WANAOHAMA DAR KUPEWA BARUA ZA UTAMBULISHO..!!!
MKOA wa Dar es Salaam unajiandaa kuweka utaratibu wa kuhakikisha
kunakuwa na utaratibu wa kutoa barua za utambulisho kwa wakazi wanaohama
kutoka sehemu moja kwenda nyingine, ikiwa ni mkakati wa kudhibiti
uhalifu hususani wizi na unyang’anyi.
Utaratibu huo utakuwa ukisimamiwa na viongozi wa serikali za mitaa
kutoa barua hizo ambazo zitakuwa na taarifa za tabia za mkazi huyo huko
alikotoka kabla ya kupokewa eneo analotaka kuhamia.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda alisema wameamua kuandaa utaratibu huo ili kupunguza matukio ya
wizi ambayo yamekithiri katika maeneo mbalimbali jijini humo.
Aliongeza kuwa hapo awali waliwataka wenyeviti wa mtaa kuwatambua
wananchi wao na shughuli wanazozifanya lakini kuna baadhi ya wananchi
wamekuwa hawataki kutambuliwa hivyo kuanza kwa utaratibu huo kutawezesha
wenyeviti kuwatambua watu hao kabla ya kupokelewa katika maeneo yao.
chanzo: swahilinews.co.tz
0 comments: