ZISINGE KAMATWA ALI SHABAB WANGETISHA .....!
Boti ya silaha zinazoaminiwa ni za ash Shabab yakamatwa na askari wa Australia
Vyombo vya habari vya Australia vimeripoti
kuwa, maafisa usalama wa nchi hiyo wamekamata boti ya uvuvi iliyokuwa
imejaa silaha zilizokuwa zinapelekwa kwa wanamgambo wa ash Shabab nchini
Somalia.
Kikosi cha majini cha
Australia kimethibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, boti hiyo
imekamatwa wakati wanamaji wa nchi hiyo walipokuwa wanafanya doria
katika eneo lililoko nje ya fukwe za Oman kwa ajili ya kulinda vyombo
vya baharini visitekwe na maharamia. Askari hao wa Australia waliitilia
shaka boti hiyo na walipoipekuwa walipata kiwango kikubwa cha silaha
ambazo inaaminika zilikuwa zinakwenda kwa wanamgambo wa ash Shabab wa
nchini Somalia. Kwa mujibu wa vyombo hivyom boti hiyo imekamatwa na kikosi cha MHAS Darwin, yapata kilimita 314 nje ya fukwe za Oman, na hiyo inahesabiwa kuwa ni shehena kubwa zaidi ya silaha kuwahi kukamatwa katika eneo hilo. Silaha hizo zilikuwa zimefichwa katikati ya nyavu za kuvulia samaki.
Wakati huo huo habari kutoka Somalia zinasema kuwa, zaidi ya watu 150 wameuawa katika shambulio la ndege ya Marekani isiyo na rubani mwishoni mwa wiki. Wizara ya Ulinzi wa Marekani, Pentagon inadai kuwa watu hao walikuwa ni wanamgambo wa ash Shabab.
Msemaji wa Pentagon, Kepteni Jeff Davis alidai jana kuwa, shambulio hilo lilifanyika siku ya Jumamosi katika kambi moja ya wanamgambo wa ash Shabab yapata kilomita 195 kaskazini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Ingawa Marekani inadai kushambulia wanamgambo wenye silaha katika nchi za Somalia, Afghanistan, Pakistan, Libya, Iraq, na Yemen, lakini wahanga wakuu wa mashambulio hayo ni raia wa kawaida
chanzo:http://parstoday.com
0 comments: