Wanawake Waislamu wa Kishia na Kisuni nchini Marekani wafanya kongamano la pamoja

...................
Wanawake wa Kiislamu wa madhehebu za Shia na Suni katika jimbo la Ohio nchini Marekani wamefanya kongamano maalumu ili mbali na kuzidi kuelewana, kuonesha kuwa masuala yanayowaunganisha pamoja ni mengi zaidi kulinganisha na wanayohitilafiana.
Wanawake hao wa Kiislamu aidha wanafanya jitihada za kuungana pamoja kukabiliana na mielekeo ya kufurutu mpaka na kutangaza ujumbe wa amani wa Uislamu.
Golchin Ozer, mtafiti wa taarifa za kitabibu katika Chuo Kikuu cha jimbo la Ohio, ambaye aliwakilisha jamii ya Waislamu wa Kisuni amesema sauti za misimamo ya kufurutu mpaka zinasikika kila mara katika vyombo vya habari, lakini wanawake Waislamu walioko nchini Marekani wanaishi kwa kufuata njia ya kadiri na wastani.
Ozer ameongeza kuwa Mashia na Masuni wanafanana katika mambo mengi kuliko wanayotafautiana na kwamba wanawake Waislamu wanataka kutilia mkazo juu ya nukta hizo za pamoja.
Aysar Hamoudi, tabibu mstaafu wa jamii ya waislamu wa Kishia kutoka mji wa Dublin amesema, akthari ya wanaoathirika na jinai za kundi la kigaidi la Daesh ni Waislamu, na kwamba magaidi hao hawana dini yoyote kwa sababu mtu anayemwamini Mungu hawezi kufanya jinai kama hizo. Hamoudi ameongeza kuwa hakuna dini yoyote inayofunza mtu kuchukia ndugu zake, wananchi wenzake na binadamu kwa ujumla; na Uislamu ni dini ya udugu...


chanzo: http://parstoday.com
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: