HILI LA FERGIE LINAUKWELI.....?

...................

Sir Alex Ferguson amemtaja Cristiano Ronaldo kama "mchezaji soka wa kipekee" bora zaidi wa kizazi chake

Ronaldo alitazamwa na Ferguson, na hatimaye alimaliza ukame wa mataji katika nyanja ya kimataifa, kuisadia Ureno kutwaa ubingwa wa Euro 2016 Jumapili.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid ambaye anapewa nafasi kubwa kutwaa tuzo ya Ballon d'Or alicheza dakika 25 tu za mechi ya fainali, akitolewa nje baada ya kupata majeraha baada ya kugongana na Payet, mechi hiyo ilienda hadi dakika za nyongeza ambapo Ureno ilishinda 1-0 dhidi ya Ufaransa.
Na Ferguson, ambaye alimleta Ronaldo Old Trafford 2003 amesisitiza kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alikuwa na shauku ya kufanya vizuri na ameng'ara.
"Ni mchezaji mwenye mwamko katika soka, Cristiano daima ni mtu anayependa kufanikiwa," Ferguson aliliambia Bild. "Daima anapenda kuwa bora, kushinda. Anapendelea zaidi mechi kubwa.
"Wakati wa kipindi changu Manchester United, Cristiano alikuwa mchezaji aliyeendelea zaidi. Kwa kufanya mazoezi kwa bidii.
"Alidumu katika mazoezi ya kupiga mashuti, kwa mguu wa kulia, kushoto, kuruka vichwa na kadhalika. Ufanisi wake ni wa ajabu. Na kama inavyoonekana leo, soka ni mchezo wa nguvu na wa kasi.
"Kwa kawaida wachezaji bora huweza kucheza miaka mitano au sita katika kiwango cha juu zaidi, kisha imekwisha." Aliongeza Ferguson. "Cristiano Ronaldo amefanya hivyo kwa miaka 10 sasa.  Hili linamfanya kuwa wa kipekee.
"Kila kizazi kina mchezaji wake wa pekee, wa sasa ni Cristiano."
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: