DARUBINI KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI HII HAPA......!
China yaanzisha darubini kubwa duniani
China
imeanzisha Jumapili hii darubini kubwa duniani katika mkoa wa Guizhou,
kusini magharibi mwa nchi hiyo. Kikiwa na mduara wa mita 500, chombo
hiki cha uangalizi kitaweza kunasa ihara mbalimbali katika pembe zilizo
mbali sana ulimwenguni.
Beijing ina matumaini kuwa ina uwezo wa kupata dalili za maisha yaliyo mbali na sayari ya dunia.
Darubinihii
kubwa duniani meanza kufdanya kazi Jumapili hii kusini magharibi mwa
China, kama sehemu ya mradi mkubwa ambapo lengo lake, kwa mujib wa
serikali ya Beijing litakua kuchunguza maisha yaliyojaa akili mbali na
sayari ya dunia.
Darubini hiyo iliyoitwa na wanasayansi kuwa ni
"Five-hundred-metre Aperture Radio Telescope" (FAST), darubini hii
imeanza kufanya kazi Jumapili hii mchana, shirika la habari la Xinhua
limearifu. Ufunguzi wake rasmi utafanyika Ijumaa 30 Septemba.
Chombo
hiki kikubwa, ambacho kinawakilisha sayari yenye mduara wa mita 500,
ukiwa sawana viwanja 30 vya soka, kimewekwa katika eneo la kijijini la
jimbo la Guizhou,kati ya vijiji vitatau vya Karst. Pamoja na kioo chake
kikubwa kinachoundwa na vifaa 4450,kitakacho kuwa na uwezo wa kuchukua
ishara kutoka pembe za mwisho wa ulimwengu.
Chombo hiki ambacho kimeanzishwa na kuanza kujengwa mwezi Machi 2011, kiligharibu 165,000,000
source: http://sw.rfi.fr

0 comments: