WAMAREKANI WEUSI WAWEKA HISTORIA
Barack Obama azindua jumba la makumbusho ya histoira ya raia wa Marekani wenye asili ya Afrika
Rais wa Marekani Barack Obama amezindua Jumamosi jumba la makumbusho ya historia ya raia wa Marekani wenye asili ya Afrika Septemba 24 mjini Washington.
Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa jumba hilo la
makumbusho, watu takriban 7 000 walihudhuria katika hafla hiyo kutoka
katika maeneo tofauti nchini Marekani.
Tukio hilo litaacha athari kubwa katika historia kwa kuwa Barack Obama ni rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuongoza nchi.
Jumba
hilo la makumbusho lililkuwa likiombwa na jamii ya wamarekani wenye
asili ya Afrika tangu mwaka 1950 na ujenzi wake kuruhusiwa na rais
George Bush mwaka 2003.
Mwanamuziki kutoka Afrika Magharibi kwa
jina la Angelique Kidjo alifungua tamasha hilo kwa kutumbiza akifuatiwa
na Stevie Wonder na PattiLaBelle.
Katika hotuba yake rais Obama
alifahamisha kuwa jamii ya wamarekani wenye asili ya Afrika walichangia
kwa kiasi kikubwa ujenzi wa Marekani
chanzo: http://www.trt.net.tr

0 comments: