JE! HIKI NI KITUKO AU ........NGURUWE WAPELEKWA BUNGENI
Nguruwe wawili mbele ya Bunge la Uganda, mjini Kampala
Alhamisi
hii nchini Uganda, wanaharakati wamepeleka nguruwe mbele ya Bunge la
Uganda katika mji mkuu, Kampala, kupinga dhidi ya uamuzi uliyopitishwa
wa kufidia wabunge nchini humo.
Ilibainika wiki hii kwamba fedha zilizotengwa katika bajeti ya taasisi hiyo ili kufidia gharama za mazishi kwa wabunge.
Takriban Dola elfu kumi na tano zimetengwa kwa kila mazishi.
Baadhi ya wabunge wametetea mpango huo.
Baadhi
ya wabunge wamesema kwamba huduma ya mazishi ya askari waliokufa
wakilihudumia taifa yanalipwa na serikali na kwamba wabunge wanapaswa
kupewa huduma kama hiyo.
Bunge
nchini Uganda linatarajiwa kutumia Dola za Marekani 177,000 kuwatuza
medali wabunge 1,200 waliohudumu katika bunge la nchi hiyo kati ya mwaka
1962 hadi 2012.
Vyombo vya Habari nchini humo vinaripoti kuwa
sherehe za kuwatuza wabunge hao zitafanyika mwishoni mwa mwezi huu
katika maadhimisho ya miaka 50 ya Bunge hilo.
Hatua hii imekuja
baada ya Gazeti la serikali ya New Vision kutangaza kuwa bunge limepanga
kutumia fedha hizo kufanikisha shughuli hiyo.
Hata hivyo raia wa
Uganda, wameonekana wakipinga matumizi ya fedha hizo katika sherehe hizo
wakati huu raia wa nchi hiyo wakiendelea kukabiliana na hali ngumu ya
kiuchumi.
Wabunge 13 wamefariki dunia kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita
chanzo: http://sw.rfi.fr/
0 comments: