Viongozi wa EAC wakubali mapendekezo ya mratibu wa mazungumzo ya Burundi
Wakuu
wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, wameiomba Jumuiya ya kimataifa
kusaidia na kufadhili mchakato wa mazungumzo ya amani kuhusu Burundi,
wakati huu wakiidhinisha mapendekezo ya mratibu wa mazungumzo hayo Rais
wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, wakati wa kuhitimisha mkutano maalumu wa wakuu wa
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais wa Tanzania na mwenyekiti wa
Jumuiya hiyo, John Pombe Magufuli, amesema wanaunga mkono juhudi za
mratibu wa mazungumzo hayo na mpatanishi wa mgogoro wa Burundi, Rais wa
Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais Magufulu amesema kuwa, walipokea taarifa ya mratibu wa mazungumzo ya amani ya Burundi, Rais Mkapa, ambaye tayari ameshazikutanisha pande zinazokinzana nchini Burundi katika mazungumzo aliyoyafanya jijini Arusha na Brussels.
Mwenyekiti huyo akaongeza kuwa, baada ya kuisoma na kuisikia ripoti ya mratibu iliyokuwa na mapendekezo kadhaa kuhusu kufikia suluhu ya mzozo wa Burundi, Rais Magufuli amesema wakuu hao wa nchi kwa kauli moja wameridhia mapendekezo yake na kwamba yametoa na kuwapa picha halisi kuwa amani inakaribia kupatikana nchini humo.
Viongozi hao wameitaka Jumuiya ya Kimataifa ukiwemo umoja wa Ulaya, kusaidia kifedha mchakato wa mazungumzo hayo, ambayo wamesema bila ya uwezeshwaji wa kutosha huenda wasifikie malengo, huku wakisisitiza imani yao kwa mratibu wa mazungumzo na hatua ambazo ameshazichukua hadi sasa.
Kuhusu Sudan Kusini, wakuu hao wa nchi wameipokea rasmi kama mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika mashariki ambayo sasa itakuwa inashiriki kwenye vikao cha maamuzi ya juu ya wakuu wa nchi.
Hata hivyo viongozi hao wamesema licha ya kufurahishwa na hatua hiyo, wanaguswa na kilichotokea mwezi Julai mwaka huu, ambapo vikosi vya Serikali vilikabiliana na vile vya waasi wanaoongozwa na aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais Riek Machar.
Viongozi hao wametaka kukomeshwa kwa mapigano nchini humo, ambapo wamezitaka pande zinazokinzana kuweka mbele maslahi ya wananchi, na kuleta amani kwenye taifa hilo kwa ustawi wa taifa hilo changa kabisa barani Afrika.
chanzo:http://sw.rfi.fr/

0 comments: