DARAJANI WAPATA BONGE LA DILI...HILI HAPA
Klabu ya Chelsea yenye makao makuu yake London England leo October 13 2016 imeingia mkataba wa na kampuni ya vifaa vya michezo ya kimarekani Nike kwa ajili ya kuanza kuidhamini kuanzia msimu ujao, mkataba huo wa Chelsea na Nike umeweka rekodi ya kihistoria klabuni hapo.
Nike wameripotiwa kuingia mkataba wa udhamini na Chelsea
katika kipindi cha miaka 15, mkataba ambao utawafanya walipwe pound
milioni 60 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 155, mkataba huo
utawafanya Chelsea wavune jumla ya pound milioni 900 katika kipindi cha miaka 15 ambazo ni zaidi ya Tirioni 2 za kitanzania.
chanzo: http://millardayo.com

0 comments: