Afrika Kusini yaanzisha mchakato wa kujiondoa ICC
Baadhi
ya nchi za Afrika zimeanza kujiondoa katika uanachama wa Mahakam ya
Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC). Siku nne baada ya rais wa Burundi
kusaini sheria ya kuindoa nchi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya
Uhalifu wa Kivita, Afrika Kusini imeanzisha mchakato wa kujiondoa kutoka
uanachama wa mahakama hiyo.
Afrika
kusini imechukua uamuzi wa kuanzisha mchakato huo kufuatia shinikizo
ilikumbana nazo mwaka uliopita kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu
wa Kivita za kuitaka imkamate rais wa Sudan Omar al Bashir wakati wa
mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg.Serikali ilijaribu kukata rufaa uamuzi wa Mahakama Kuu ikisema Bashir alikuwa na kinga ya urais kwa sababu yeye ni kiongozi wa taifa.
Lakini Jaji Hans Fabricius alisema rufaa hiyo haiwezi kufanikisha chochote.
“Afrika Kusini ni mwanachama wa Mkataba wa Roma uliounda Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, na mkataba huo unabatilisha sheria zote ambazo huenda zingempa kinga Bashir asikamatwe na kushtakiwa”, amesema Jaji Hans Fabricius.
Kiongozi huyo wa Sudan amekuwa akisakwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya halaiki na makosa ya uhalifu wa kivita Darfur.
Omar ala Bashiri aliyechukua mamlaka kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 amekuwa akisakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya halaiki na makosa ya uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur, madai ambayo Bw Bashiri amekanusha.
Itafahamika kwamba nchi nyingi za Afrika zinailaumu ICC kwa kuzilenga zaidi nchi za Afrika
chanzo: http://sw.rfi.fr/afrika/

0 comments: