RAIS KABILA APATA SHAVU TENA,
Mahakama yaridhia Kabila kuendelea madarakani
Mjini Kinshasa leo (18.10.2016)vyama vinavyoshiriki
katika serikali vimetia saini makubaliano yanayotoa ruhusa kuchelewesha
uchaguzi uliotarajiwa kufanyika katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
mwezi ujao.
Vyama vinavyounda muungano tawala katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo na vyama vingine vidogo vimekubaliana kuchelewesha uchaguzi wa
mwezi ujao hadi Aprili mwaka 2018. Vyama hivyo vimetia saini
makubaliano hayo mjini Kinshasa leo(18.10.2016). Makubaliano hayo
yanatoa nafasi kwa Rais Joseph Kabila kusalia madarakani hadi uchaguzi
mpya utakapofanyika.Mkataba huo ulipitishwa baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa takriban siku 40, chini ya usimamizi wa mjumbe wa Umoja wa Afrika Edem Kodjo, licha ya kususiwa na vyama muhimu vya upinzani, kikiwemo UDPS cha kinara wa upinzani Etienne Tshisekedi. Makubaliano hayo hayafafanui iwapo rais Kabila anaweza kuwania muhula mwingine baada ya mwaka huo.
Vyama ambavyo havikushiriki katika majadiliano hayo vinadai kwamba Rais Kabila kubaki madarakani kupindukia muda wake anaoruhusiwa na katiba ni kukiuka katiba ya nchi hiyo.
chanzo"dwswahili

0 comments: