MAIMAMU WATATU WAHUKUMIWA KUNYONGWA
Mahakama ya kijeshi yawahukumu Maimamu 3 adhabu ya kifo
Mahakama
ya kijeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewahukumu
watu saba, ikiwa ni pamoja na Maimamu watatu, adhabu ya kifo. Watu hao
wanashtumiwa kushirikiana na waasi wa Uganda wa kundi la ADF-Nalu.
Uamuzi
huu ni wa kwanza kutolewa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi
ya watu wanaotuhumiwa kushirikiana na kundi la waasi wa Uganda
linaloundwa kwa idadi kubwa na Waislamu na ambalo limekua likiendesha
harakati zake katika ardhi ya Congo.Hukumu hii imetangazwa na Mahakama ya Juu ya kijeshi nchini DRC, katika wilaya ya Beni, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa vyanzo mahakama.
Gilbert Kambale, kiongozi wa shirika la kiraia wilayani Beni, amekaribisha uamuzi huo dhidi ya watuhumiwa saba.
"Tunakaribisha uamuzi huu kwa sababu tunaamini kwamba ukweli umethibitika. Watuhummiwa wana uhusiano na waasi hao, yaani kundi la waasi wa Uganda la ADF-Nalu. Tunaamini kwamba mahakama imefanya kazi yake" amesema Bw Kambale.
Viongozi wa jamii ya Waislamu wilayani Beni wamejizuia kuzungumza kuhusu uamuzi huo.
Si rahisi kukata rufaa kwa uamuzi wa mahakama ya kijeshi nchini Congo.
Kwa miaka kadhaa, adhabu ya kifo haitekelezwi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kundi la waasi la ADF-Nalu linatuhumiwa kutekeleza mauaji ya mara kwa mara wilayani Beni katika miaka miwili iliyopita
Chanzo: http://sw.rfi.fr/afrika

0 comments: