UNAWEZA KUJIBU MASWALI HAYA JUU YA KUPIGWA MWANAFUNZI MBEYA DAY

...................
Anaandika Mathias Canal Wa Iramba-Singida
Maswali ya Kiutafiti: Sakata la Mbeya Sec.
Kaka yangu Creptone Madunda haungi mkono kilichofanywa na Walimu kule Mbeya Sec ila ameamua kuniunga mkono kutafuta chanzo cha tukio ili tujue matokeo ya kadhia hiyo.
Taarifa zinasema Seba (Mwanafunzi) na wenzake hawakufanya zoezi la Kingereza lililotolewa na Mwl. Msigwa. Mwalimu aliamua kuwapa adhabu (nadhani ya kawaida) wanafunzi wote ambao hawakufanya zoezi hilo. Wote walikubali adhabu isipokuwa bwana Seba ambaye alionesha kugomagoma.. Taarifa ya Waziri mmoja (aliyoiandika ktk ukurasa wake wa Fb) inasema Seba na Mwalim "Walishikana Koo" (Haielezi nani alianza kumshika mwenzake). Baada ya hapo Seba akapelekwa ofisini, eneo alilopewa "mkong'oto" tulioushuhudia kwenye ile video clip.
MASWALI YA KIUTAFITI,..
1. Ni kwa nini Seba pekee ndiye agomee adhabu iliyotolewa na mwalimu wakati wengine wamekubali?? What is so special with Seba? Character assessment ya Seba inasemaje?? Je ananidhamu isiyotiliwa shaka???
2. Ni kwa nini Seba alimshika Koo Mwalimu wake? Je alitaka kumpiga, kumuua au kumduru mwalimu wake? Au alikuwa anajitetea? (Kwa kuwa hakuwa na namna nyingine) Je Mwanafunzi mwenye nidhamu isiyo na shaka anaweza kumshika Koo mwalimu wake? Anaweza kugoma kisa pushapu au viboko vya kawaida tu kama walivyoadhibiwa wengine???
3. Seba aligombana na mwalimu mmoja (Msigwa) akiwa darasani, lakini video clip inatuonesha walimu wanne wakimshambulia bwana Seba akiwa Staff room/office ya walimu. Je Seba alifikaje ofisini? Yaani alitembeaje kutoka darasani mpaka ofisini? Alienda peke yake? Alipelekwa na mwalimu Msigwa au Walimu wote wanne walikuja kumbeba darasani?
4. Kama alitembea mwenyewe au Alipelekwa na Mwl Msigwa, Ilikuwaje mpaka walimu wote wanne waanze kumpiga Seba? Je aliwatukana? Walimu waliona wajifunzie kupiga hapo? Walimu wanamatatizo ya akili? Ni kwa nini wanne dhidi ya mmoja? Je Seba anamanguvu sana? Je Seba alipandisha mapepo? Au walimu wana chuki binafsi na Seba?
5. Kama walimu hawa wanamatatizo ya akili... Tangu wafike hapo wameshafanya matukio mangapi ya aina hiyo? Je yaliripotiwa wapi? Kama hawajawahi kufanya hivyo, Je imekuwaje wafanye hivyo kwa Seba tu wakati waliokosa ni wengi, wanafunzi ni wengi na tena huyo si mwanafunzi wa kwanza wao kumwadhibu. Historia ya walimu hawa (Character assessment) tangu wafike hapo shuleni inasemaje?? Je walimu hawa uhusiano wao na wanafunzi wengine pia na walimu wengine ukoje??
6. Je kuna sheria yoyote maalum inayomlinda, inayomwongoza au inayombana Mwanafunzi wa Ualimu akiwa mafunzoni? Inasemaje juu ya kosa walilofanya walimu hawa? Je kosa hili linatofautianaje na daktari anayeua mgonjwa au anayekosea tiba kwa mgonjwa akiwa mafunzoni, Au Dereva mwenye leseni ya Leaner anapomgonga mtu? Je kukosea si sehemu ya mafunzo? Kama hawatakiwi kukosea yaani wanajua, sasa ni Kwa nini wapo mafunzoni???
7. Je adhabu ya Mwalim aliyeyeko mafunzoni kama atafanya makosa ipoje?? Chuo hakina utaratibu wa kuwaadhibu wanafunzi wake wanapofanya makosa kama hayo?
Kwahiyo hapa tuna variables zifuatazo ambazo zinatuongoza kujua undani wa tukio hilo,
1. Tabia ya Seba na Profile yake
2. Tabia za Walimu (na Profile zao)
3. Wanafunzi wote ambao hawakufanya zoezi la Kingereza lililotolewa na Mwl Msigwa na walikubali kuadhibiwa
4. Wanafunzi wengine wanaofundishwa na walimu hao.
5. Walimu wote wa Shule hiyo na hasa Mkuu wa shule na Mwalim wa Malezi.
6. Utaratibu wa adhabu kwa walimu-wanafunzi unaotolewa na chuo husika
7. Sheria za nchi zinazohusiana na tukio hilo.
Kumbuka, hapa Mimi sijasema kuwa Walimu wale wameonewa wala sijasema Mawaziri waliotoa adhabu Wamekosea, aka. (Mimi ni nani hadi nipinge hayo) Mimi lengo langu ni kutafakari na kujiuliza haya maswali ambayo yanaweza kuibua mambo mengi ambayo yako nyuma ya pazia, na hivyo isiwe rahisi kuyaona. Tutafakari pamoja... Kwa Upole bila jazba wala kutumia hisia zetu ili tupate majibu yakisayansi.
My Take...!
Katika malezi na uimara wa makuzi ya mwanafunzi kuna makundi kadhaa ambayo yanatakiwa kuwa makini kuhakikisha mwanafunzi anakuwa katika weledi, nidhamu na Elimu bora.
Mosi kabisa Wazazi/Walenzi ni watu muhimu kudhibiti hulka hasi na mtazamo mbovu katika nidhamu ya mwanafunzi maana kwa muda mwingi mwanafunzi anakuwa na mzazi/mlezi kuliko MTU mwingine yeyote hivyo kama mwanafunzi akiwa na nidhamu mbovu tunapaswa kuanza kuwalaumu hawa.
Pili, Walimu wanatumia muda mwingi sana kuwa mwanafunzi huyo shule takribani masaa 8 mpaka 10 hivyo wana muda wa kugundua tabia zinazochomoza za mwanafunzi kwahiyo nategemea wana nafasi mahususi kabisa kuzikabili Tabia ovu za wanafunzi na kuzipatia ufumbuzi.
Tatu, serikali na Jamii kwa ujumla...Wakati Mimi nasoma nakumbuka kulikuwa ma msemo uliosema kuwa mtoto wa mwanao ni wa kwako. Msemo huu ulijikita kuamsha ari kwa Jamii kutambua kuwa mtoto/mwanafunzi akikosea anatakiwa kukosolewa sio kuachwa na utukutu wake.
Kuna watoto wengine walishindikana kuwakunja angali wabichi tusitegemee kuwakunja angali wamekauka.
Mwisho niseme nimesikitishwa sana na namna ambavyo mwanafunzi huyu kashambuliwa zaidi nisikitike kuwa maamuzi yamechukuliwa kwa kufukuzwa shule dhidi ya mwanafunzi ambaye hajahusika kabisa na kadhia iliyotokea. Kufanya maamuzi kwa vyombo vyenye Mamlaka ni jambo moja lakini Jambo la Pili ni kutoa maamuzi ya uchunguzi yasiyokuwa na hata chembe ya mashaka.
Salaaam...!
Mathias Canal
Mwanza
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: