AJALI YA NDEGE YAPOTEZA WATU 76 WENGI WAO NI WACHEZAJI WA TIMU YA SOKA.
kwa sasa dunia imekumbwa na tukio la nne la vifo vya wachezaji kwaajali ya ndege, tukio la kwanza la Man utd, Torino na Zambia
.
Moja kati ya habari au matukio makubwa yaliyotokea asubuhi ya November 29 2016 ni taarifa ya kikosi cha timu ya soka ya Chapecoense ya Brazil kupata ajali ya ndege wakiwa angani kuelekea kutua katika uwanja wa ndege wa Medellin.
Ndege hiyo kabla ya kuanguka katika milima ya Colombia ilianza kupotea katika rada, ndege hiyo ya shirika la ndege la Airline LaMia
imethibika kuwa ilikuwa imebeba abiria 72 na wafanyakazi 9 wa ndege,
abiria hao 72 wanaripotiwa wote walikuwa ni msafara na wachezaji wa timu
ya Chapecoense ya Brazil.
Kikosi cha timu hiyo kilikuwa kinasafiri kuelekea Colombia kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa fainali ya Sudamerican dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia
ambapo mchezo huo ungechezwa Jumatano ya November 30 2016, kati ya
watu 81 waliokuwemo katika ndege hiyo ni watu 5 ndio wametoka salama na
76 wameripotiwa kupoteza maisha.
.
MAAMUZI YA TIMU YA Atletico Nacional ya Colombia BAADA YA AJALI YA NDEGE
Klabu ya Atletico Nacional ya Colombia ambapo ilikuwa icheze mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Sudamericana kesho Jumatano ya November 30 2016 Colombia dhidi ya klabu ya Chapecoense ya Brazil imetangaza maamuzi tofauti.
Atletico Nacional ambapo ndio wangekuwa wenyeji wa mchezo huo wa fainali ya kwanza, wameomba shirikisho la soka la America Kusini (CONMEBOL) kuwa kutoa Kombe hilo kwa timu ya Chapecoense ya Brazil kama sehemu ya heshima.
Msafara wa watu 72 wa timu ya Chapecoense ya Brazil wamepata ajali ya ndege asubuhi ya leo wakiwa Colombia,
ndege hiyo imepata ajali ikiwa na jumla ya watu 81 kati ya hao watu 9
ni wafanyakazi wa ndege, katika list ya watu 81 ni watu watano tu ndio
wamefanikiwa kutoka salama.
0 comments: