KWANINI TANZANIA TU KILA SIKU....?
Tuna maswali mengi ya kujiuliza
kwanini Timu yetu ya Taifa haifanyi vizuri katika mashindano mbalimbali.
Tukijiuliza tunapata majibu mengi sana ya kweli na yakufikirika.
KUHUSU MECHI NA WAZIMBABWE NINA
YANGU YA KUSEMA
Kwanza kabisa poleni Watanzania
kwa kuendelea kuumizwa na matokeo. Lakini safari hii natoa lawama kwa Uongozi
wa mpira nikimaanisha TFF. Walichokifanya ni kutimiza wajibu na sio kufanya
sehemu ya majukumu yao ya kikazi ya kuwatumikia watanzania na kuhakikisha
tunapata ushindi.
Ni jambo la kushangaza uongozi wa
mpira Tanzania kushindwa kuweka ratiba inayoelewka ya Timu ya Taifa. Ikumbukwe kuwa FIFA hutoa ratiba yao mapema
na ndipo Mataifa mengi hupanga ratiba kwa kuzingatia kalenda ya FIFA. Ligi zote
duniani zilisimama kuweza kuipa nafasi FIFA itemize ratiba yake kwa timu za
kufuzu kombe la dunia na mechi za kirafiki.
Swali la kujiuliza
Kulikuwa na umuhimu gani wa
TAnzaia kumaliza mzunguko wa ligi katikati ya wiki wakati tuna mechi ya
kirafiki weekend?
Kwa hili wachezaji hawajapumzika
wala hawaja kaa kambini kuweza kutengeneza good chemistry kwaajili ya mechi na
wazimbabwe. Kulikuwa na haja gani kumaliza mzunuko , kasha kucheza mechi ya
kimataifa na kupumzika kwa maana ya mapumziko baada ya mzunguko wa kwanza? Kwanini
tusinge ipa timu ya Taifa muda wa wiki mbili kasha ligi yetu tukamalizia
weekend ijayo kasha tupumzike? Au zengwe kwa kocha aonekane ameboronga kasha tumtimue?
Kwa upande mwingine Tanzania
mpira sio fani yetu ama viongozi wa mpira wapo kwaajili ya kuionyesha dunia
kuwa na sisi tunashiriki mpira wa miguu.
Kama kweli Tunataka kupata
maendeleo ya mpira basi tujifunze zaidi ama tulete mkoloni atutawale tena
kwenye mpira tu pengine tutapata mwelekeo lakini kwa tulipo sasa hali ni tete

0 comments: