SERIKALI KUNUNUA NDEGE ZA KISASA KUIMARISHA ULINZI HIFADHI ZA TAIFA

SERIKALI imepanga kununua ndege za kisasa ili kuimarisha ulinzi katika Hifadhi za Taifa nchini.
Hayo
 yamesemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja 
Jenerali Gaudence Milanzi wakati akihojiwa na kipindi maalumu cha 
TUNATEKELEZA kinachorushwa hewani na kituo cha Televisheni ya Taifa 
(TBC1).
Meja
 Jenerali Milanzi anasema Serikali imeweka mfumo maalumkatika  kulinda 
hifadhi zilizopo na ili kuweza kukabiliana na ujangili unaojitokeza 
katika hifadhi mbalimbali nchini.
“Sekta
 ya Utalii nchini inachangia pato la taifa kwa takribani asilimia 17.5 
na kutoa ajira kwa zaidi ya watumishi milioni 3 katika sekta mbali mbali
 ya utalii nchini, hivyo ni vyema tukaweka mikakati madhubuti katika 
kulinda vyanzo vilivyopo” alisema Meja Milanzi.
Aidha,
 alisema kuwa Serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria 
watu wote watakaobainika kujihusisha na ujangili pamoja na biashara ya 
magogo ili kulinda hifadhi za Taifa na kuweza kuvutia watalii nchini.
Aidha
 Meja Jenerali Milanzi aliitaka jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa 
kutumia nishati mbadala ili kulinda misitu iliyopo kwa kutunza mazingira
 na hifadhi za taifa.
Mbali
 na hayo Meja Jenerali Milanzi alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi 
zinazovutia watalii wengi kutoka Marekani na Uingereza hivyo kuwataka 
wananchi kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamimia Hifadhi za Taifa 
ili kuzudi kuvutia watalii nchini.chanzo:maswablog
0 comments: