WAZIRI MKUU AMTAKA WAZIRI MWAKYEMBE KUJIELEZA NDANI YA SIKU SABA

Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amempa siku saba Waziri wa Katiba na Sheria Dr.
Harrison Mwakyembe kutoa maelezo ya kwanini Tanzania haijakamilisha
mkataba wa mawakili wa Afrika Mashariki, mkataba ambao
unafanya kutambuana katika utendaji wao wa kazi.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo wakati akimuwakilisha Rais Magufuli katika
mkutano wa 21 wa mwaka unaojumuisha chama cha wanasheria wa Afrika
Mashariki uliofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius
Nyerere jijini Dar es salaam.
“Nimeshtushwa
kidogo na maelezo kwamba mkataba huu unasubiri tu kusainiwa na
wanasheria wakuu wa nchi wanachama, ili uanze kufanya kazi katika nchi
zote za jumuiya isipokuwa Tanzania. Natumia nafasi hii kukuagiza waziri
uniletee taarifa ofisini kwangu ndani ya wiki moja mnieleze ni kwanini
mkataba huu hamkukamilisha kwa kuiingiza Tanzania” – Waziri Mkuu Majaliwa
chanzo:Ayo Tv

0 comments: