UNATAKA UFADHILI WA MASOMO AU MTAJI WA BIASHARA
Kama wewe
ni mmoja wa wanaotafuta ufadhili wa masomo au msaada wa kifedha ili ujiendeleze
kielimu au kibiashara , basi makala hii inakuhusu sana.
Katika makala ya MAMBO 4 YA MSINGI ILI KUPATA SCHOLARSHIP YA ELIMU
nilitaja mambo
ya kuzingatia ili kupata schorlaship. Hata hivyo kuna jambo moja nimeliona
likijirudia mara kwa mara na ambalo sikulitaja katika makala ile. Nakushauri
ukaisome ile makala yote vizuri pia. BOFYA HAPA KUSOMA HAYO MAMBO 4
Kupata
ufadhili wa masomo kunaanzia katika kujiweka katika mazingira ya kuanzisha na
kuendeleza mawasiliano na watu maalum ambao wanaweza kukupatia huo ufadhili wa
masomo au mtaji wa biashara.
Kuna namna
nyingi ya kuwapata watu wanamna hiyo. Katika makala nyingine tutajadili jinsi
ya kujijengea mazingira ya kukutana na watu wanaoweza kuwa wafadhili wako. Leo
tujifunze jambo la msingi zaidi ili hata ukikutana nao uweze kuwakamata kuwa
wafadhili wako.
Katika
makala hii nataka nikusisitize swala hili la msingi la Kuweza Kufanya
Mawasiliano Fasaha. Jambo hili ni dogo ila ukilipatia vizuri litakujengea fursa
kubwa hata kama una mapungufu katika baadhi ya maeneo.
Ninaposema
kufanya mawasiliano fasaha namaanisha
yafuatayo:
Tafuta kujisikia
kuvutiwa na mtu unayewasiliana nae:
Watu hufanya
mawasiliano na watu ambao wanaonekana kutaka kufanya mawasiliano. Penda
kumuachia nafasi mtu unayewasiliana nae ili akupashe yaliyo yake. Onyesha
kutaka kufahamu zaidi kwa kuuliza maswali na kukumbuka anayokuambia. Onyesha
kuwa unajali na kuwa upo tayari kusikiliza zaidi na zaidi.
Kuwa mwenye
kujua vitu vingi:
Wewe pia
unahitaji kuwa mwenye mazungumzo yanayovutia. Uwe na uwezo wa kuchanganya
mazungumzo ya namna nyingi kutegemea na aina ya mtu unayewasiliana nae iwe ni
mambo ya kiimani, siasa, burudani, habari za kitaifa, kimataifa, michezo,
vichekesho na hata ya fani husika.
Jua
anayojua au kupendelea mtu unayewasiliana nae:
Mara nyingi
katika mawasiliano tunajikuta tuna shauku ya kujielezea sisi wenyewe, mambo
yetu na jinsi tulivyo bora kiasi cha kupoteza nafasi ya kusikia na kujifunza
nini mtu mwingine anajua , anafuatilia na kupendelea. Mfano ukijua vitu
anavyopendelea na yapi anafahamu au anajifunza mtu unayewasiliana nae, ni rahisi
nawe kujifunza hayo mambo au kufuatilia ili uwe na yapi katika kuendeleza
mawasiliano yaliyo na mvuto kwa mtu husika.
Kwa namna
gani hii itakusaidia ?
Uwezo wako
wa kuwasiliana kwa ufasaha na kuendeleza mawasiliano kutamfanya mhusika
unayetaka akupe ufadhili wa masomo au mtaji akufahamu vizuri na avutiwe nawe.
Na ni rahisi mtu kutoa ufadhili kwa mtu anayempenda na kumjali. Hivyo kwa
kutengeneza mawasiliano bora unajifanya “promo” kuwa wewe unafaa kusaidiwa. Na
ni promo ya ukweli kwani mfadhili anapata kukufahamu vya kutosha na yeye mwenyewe
kujikomit kukusaidia.
Hitimisho:
Katika mazungumzo yako usiweke mbele kutangaza shida zako au kuomba msaada wa
ufadhili wa elimu au mtaji wa biashara. Fanya mazungumzo kwanza, jenga
mahusiano. Muache muhusika mwenyewe ajisikie hitaji la kukusaidia. Na kama mhusika
ana uwezo kweli, na mmejenga uhusiano mzuri, wala usihofu, kwani marafiki
husaidiana. Atakusaidia tuu.
chanzo: http://mbuke.blogspot.com.co

0 comments: