MJENGO WA HITLER KUTWALIWA NA SERIKALI

...................
Bunge nchini Austria limepitisha sheria inayotoa fursa ya kutwaa nyumba ambapo kiongozi wa zamani wa Ujerumani Adolf Hitler alizaliwa mwaka 1889.
Mmiliki wa sasa wa nyumba hiyo Gerlinde Pommer amekataa mara nyingi kuuza nyumba hiyo inayopatikana Braunau am Inn.
Amekataa pia kukubali ifanyiwe ukarabati.
Bi Pommer sasa atalipwa fidia na nyumba yake itwaliwe.
Lakini haijabainika serikali itafanyia nini nyumba hiyo ambayo zamani ilitumiwa kama mgahawa.
Serikali hata hivyo imeonyesha nia ya kutaka kuzuia nyumba hiyo kuwa kivutio kwa watu wanaofuata sera za Wanazi.
Uamuzi huo wa bunge utafikisha kikomo mzozo wa muda mrefu kati ya serikali na Bi Pommer, ambaye kwa sasa amestaafu

zaidi habari hii inapatikana hapa bbc.com/swahili/habari
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: