Afungwa miaka 16 kwa ubakaji Afghanistan
Afisaa mmoja wa polisi nchin
Afghanistan amehukumiwa kifungo cha miaka 16 gerezani kwa kumbaka
msichana mwenye umri wa miaka kumi na nane.
Msichana huyo alitekwa nyara na kundi la
maafisa wa polisi wa Afghanistan na baadaye alipigwa na kubakwa katika
kipindi cha siku tano mnamo mwezi Mei mwaka huu.Waandishi habari wanasema kesi hiyo siyo ya kawaida kwa kuwa mwanamke huyo ndiye aliyeripoti kisa hicho.
Vyombo vya habari vya kimataifa vimeangazia mashtaka yake na kumfanya rais Karzai kuagiza uchunguzi wa uhalifu. Maafisa wengine watatu wa polisi pia walihukumiwa kwa kuhusika na ubakaji huo.
chanzo:bbcswahili
0 comments: