RAIS BARACK OBAMA KUTUA TANZANIA TAREHE 1 JUNE 2013
Imeelezwa kuwa ujio wa Rais Barack Obama
wa Marekani nchini, ni fursa nyingine kwa Tanzania kukuza uchumi na
kuimarisha uwekezaji.
Hata hivyo, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni mchumi kitaaluma, amesema kuwa ujio
wa Rais Obama unaweza kuleta neema hasa kama atakuwa ameambatana na
wataalamu wa masuala ya maendeleo.
Hii itakuwa ziara ya pili ya Rais Obama katika Bara la Afrika.
Hii itakuwa ziara ya pili ya Rais Obama katika Bara la Afrika.
Ziara
yake ya kwanza aliifanya wakati wa awamu yake ya kwanza madarakani,
wakati ziara ya safari hii ni kipindi chake cha lala salama.
Rais
Obama alianza rasmi awamu yake ya kwanza kama Rais wa Taifa kubwa,
Januari 20, 2009, wakati ng’we yake ya mwisho ilianza Januari 21, 2013.
Rais
Obama anatarajiwa kufanya ziara hiyo mwishoni mwa Juni mwaka huu,
ambapo Tanzania itakuwa miongoni mwa nchi za mwanzo za Afrika Mashariki
kutembelewa na kiongozi huyo.
Ziara ya Rais Obama
inafanyika baada ya ziara ya Rais Xi Jiping wa China aliyeitembelea
Tanzania Machi 28, mwaka huu, ambapo Tanzania ilikuwa nchi yake ya
kwanza kuitembelea kwa Afrika tangu achaguliwe kuwa rais, Machi 14,
2013.
Akizungumzia ziara hiyo tarajiwa, Mwenyekiti wa Taifa wa
Chama cha Wananchi (Cuf), Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni mchumi,
alisema amani, utulivu na uimara wa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi
kwa kulinganisha na nchi nyingine za jirani, vimechangia kuwapo kwa
ziara hiyo.
Profesa Lipumba alisema pia ugunduzi wa
rasilimali za asili kama vile gesi, mafuta na madini ya urani ni sababu
nyingine iliyomfanya Rais huyo kuja nchini.
Hivyo aliwashauri viongozi wa Serikali kujipanga kwa ajili ya kufungua mlango huo mwingine wa uchumi na uwekezaji.
Alisema
pamoja na hali hiyo pia kuna mambo ambayo yanaweza kuchafua taswira ya
nchi kama vile ubovu wa miundombinu ya barabara, msongamano wa magari
barabarani na msongamano wa meli bandarini wakati zikisubiri kushusha
mizigo.
Jumatano ya wiki hii, Waziri wa Mambo ya Nje wa
Marekani, John Kerry alitangaza mbele ya wajumbe wa Kamati ya
Ushirikiano kati ya Marekani na Afrika, kwamba Rais Obama hivi karibuni
atafanya ziara Afrika.
Ingawa Kerry hakutoa maelezo
zaidi ya nchi gani za Afrika ambazo Rais Obama atazitembelea, lakini
baadhi ya vyombo vya habari vya Nigeria vilieleza kiongozi huyo atafanya
ziara Tanzania, Rwanda na Nigeria.
Kiongozi wa kwanza wa Afrika kukutana na Rais Obama
tangu awe Rais wa Marekani, alikuwa Rais Jakaya Kikwete aliyekutana naye
Mei 2009, Washington, Marekani.
Kwa nini ni Tanzania na Rwanda
“Kenya
asingeweza kwenda kutokana na suala la Rais na Makamu wake kutuhumiwa
kuhusika katika mauaji ya kimbari yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu
2007/2008, kwani msimamo wa Marekani ni kutaka wahusika wa vitendo vile
wakamatwe na kufikishwa mahakamani. Hivyo kwake kuwatembelea watuhumiwa
asingeeleweka,” alisema Profesa Lipumba.
Alibainisha
kuwa Rwanda ina uhusiano wa karibu na Marekani na pengine suala la
mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) litachukua nafasi.
Kulingana
na taarifa za Ikulu ya Marekani, Rais Obama alikuwa amepanga muda wake
mwingi wa awamu ya pili ya uongozi wake kujihusisha na masuala ya
Afrika ( Chanzo: mwananchi)
Uthibitisho wa Habari hizi pia ni kutokakana na kutangazwa kwenye BBC NEWS WORLD zikithibitisha siku ya Rais wa Marekani, Barack Obama kuja Tanzania itakuwa ni tarehe 1/06/2013
Uthibitisho wa Habari hizi pia ni kutokakana na kutangazwa kwenye BBC NEWS WORLD zikithibitisha siku ya Rais wa Marekani, Barack Obama kuja Tanzania itakuwa ni tarehe 1/06/2013
0 comments: