UTAMBULISHO WA USIKU WA HIP HOP & FAINALI ZA VODACOM MIC KING KWA WANAHABARI
Wednesday, May 22, 2013
Meneja Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho (wa pili kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo. Wengine pichani kutoka kushoto ni DJ John Dilinga (JD), Prodyuza Ally Baucha na Prodyuza Tudd Thomas.
Kutoka kushoto waliokaa ni msanii Stamina, DJ John Dilinga, Abdallah Mrisho, Ally Baucha na Tudd Thomas katika picha ya pamoja na washiriki wa The Vodacom Mic King waliosimama nyuma.
Wakali wa MIC wanaowania gari wakiwa katika pozi na gari hilo.
Wanahabari wakichukua baadhi ya matukio.
...Wakimsikiliza Abdallah Mrisho.
Hawa ndiyo wakali tisa wanaowania gari aina ya Toyota Funcargo (New Model).
-
Uongozi wa Dar Live Co. Ltd leo
umetambulisha tamasha kubwa la kila mwaka la Usiku wa Hip Hop na fainali
za kumtafuta Mkali wa Mic zijulikano kama 'The Vodacom Mic King' kwa
wanahabari. Tamasha hili litafanyika Jumamosi hii, Mei 25, 2013 katika
Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini
Dar. Jumla ya vijana tisa wenye vipaji watapanda stejini kuchuana na
mshindi ataondoka na gari aina ya Toyota Funcargo (New Model) yenye
thamani ya shilingi milioni 15. Mbali na zawadi ya gari, mshindi wa
kwanza, pili na watatu, watapata fursa ya kurekodi wimbo mmoja chini ya
Prodyuza mahiri nchini, Tudd Thomas,
aliyerekodi wimbo maarufu wa Leka
Dutigite wa Kigoma All Stars na nyingine nyingi. Majaji katika shindano
hili ni mwandishi mkongwe wa habari za muziki na wasanii, Abdallah
Mrisho, DJ John Dilinga (JD) na Prodyuza Ally Baucha.
Tamasha hilo litapambwa na burudani
kutoka kwa wakali wa Hip Hop nchini ambao ni Fid Q, Joh Makini, Stamina,
Kala Jeremiah, Nay wa Mitego pamoja na shoo kali kutoka kundi la Wakali
Dancers. Katika usiku huo, zitatolewa tuzo kwa wasanii wa Hip Hop na
kwa wimbo bora wa Hip Hop uliofanya vizuri mwaka 2012/13. Kutakuwa na
Tuzo kwa Msanii Mkongwe Bora wa Hip Hop na Msanii Chipukizi Bora wa Hip
Hop pamoja na Wimbo Bora wa Hip Hop.
PICHA NA MUSA MATEJA / GPL
SOURCE; LEWIS MBONDE
0 comments: