Utapia mlo waathiri matokeo ya watoto shuleni

...................
Watoto wengi duniani wanakumbwa na tatizo la utapia mlo

Robo ya watoto wote duniani wako katika hatari ya kutofanya vyema shuleni kwa sababu ya viwango vya juu vya utapia mlo. Hii ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la misaada kwa watoto la Save the Children.
Watoto hao kwa kukosa lishe bora, uwezo wao wa kusoma na kuandika unaathirika sana.
Utafiti uliofanywa na shirika hilo uligundua kuwa watoto wenye utapia mlo hupata athari kubwa ambazo haziwezi kutibiwa , wao huwa wadogo na wasio na nguvu na hata ubongo wao haukomai vyema.
Shirika hilo linasema kuwa vingozi wa mataifa yaliyostawi kiviwanda yanapaswa kutoa kipaombele kwa tatizo la utapia mlo.
Watakutana Ireland ya Kaskazini mwezi ujao.
Ripoti hiyo,yenye mada 'Food for Thought' imetokana na utafiti uliofanyiwa maelfu ya watoto nchini, Ethiopia, India, Peru na Vietnam.
Utafiti huo unapendekeza kuwa watoto walio chini ya umri wa miaka minane, wanadumaa kutokana na utapia mlo, 19% ya watoto hao, wanaweza kwa urahisi kufanya makosa katika kuandika sentensi fupi, kama kama '' Jua ni kali'' au ''napenda Mbwa'' kuliko watoto wenye kupata lieshe bora.
"lishe mbovu kwa watoto linadunisha viwango vya uelewa katika nchi zinazostawi na pia ni kikwazo kikubwa katika kukabiliana na vifo vya watoto wachanga,'' alisema afisaa mkuu mtendaji wa shirika hilo.
Serikali ya Uingereza imeandaa mkutano mkubwa mjini London tarehe nane mwezi Juni, kabla ya mkutano wa G8 ambao unaratajaiwa kuangazia maswala kama uhaba wa chakula Afrika na haja ya nchi zinazostwi kuwa na mipangio yao ya lishe bora.

chanzo : bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: