Wataka waruhusiwe kujiua Uingereza

...................

Marehemu Tony Nicklinson naye aliwahi kutaka mahakama imruhusu auawe kwa usaidizi wa daktari kwa sababu ya ulemavu wake

Wanaume wawili wenye ulemavu mbaya zaidi wanakwenda mahakamani kukata rufaa katika kesi inayoonekana kuwa moja ya kesi inayotaka mageuzi makubwa ikitaka kubadilisha sheria za serikali kuhusu haki ya mtu kufa.
Mmoja wa watu hao, Pail Lamb amekuwa na ulemavu mbaya kwa miaka mingi pamoja na kupitia uchungu mwingi, hawezi kujitoa uhai wake na anataka madaktari waruhusiwe kumuua bila ya kukabiliwa na kosa la mauaji baadaye.
Mwanamume mwingine anayejulikana kama Martin, anataka uamuzi utakaowaruhusu madaktari wamsaidie kujiua ingawa waweze kulindwa kutokana na sheria za kuweza kuwashtaki kwa kufanya kitendo cha mauaji.
Wakosoaji wanasema kuwa ikiwa mahakama itaruhusu wawili hao wajiue, itakuwa na athari kubwa kwa watu wazee na wenye ulemavu kutaka kujinyonga ili kuzuia kuwahangaisha jamaa zao kuwahudumia

Kutoka bbcswahili http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: