WATOTO, ''WADHULUMIWA SEHEMU ZA VITA''
Shirika la kuwahudumia watoto la
Save the Children, linasema kuwa watoto ndio waathiriwa wakubwa wa
ubakaji na dhulma zengeine za kingono katika maeneo ya vita duniani.
Ripoti ya shirika hilo inazingatia data
waliokusanya pamoja na ushahidi kutoka katika nchi nyingi ikiwemo
Colombia, Liberia na Jamuhuri ya kidemorasia ya Congo.Swala hilo litajadiliwa na mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G8 au la nchi zilizostawi kiviwanda.
Uingereza ilisema kuwa itatoa kipaombele kwa swala la dhulma za kingono katika maeneo ya vita wakati wa uongozi wake wa G8 mwaka huu.
Ripoti hiyo ya Save the Children, yenye kauli mbiu, Dhulma za kinyama dhidi ya watoto, inasema kuwa takwimu kutoka katika nchi kadhaa, zilizoathirika kutokana na vita katika miaka kumi iliyopita, zinaonyesha kuwa watoto ndio hudhulumiwa zaidi kingono katika maeneo ya vita na hata baadaye.
Makovu ya kudumu
Utafiti uliofanywa nchini Liberia, ulionyesha kuwa asilimia 83 ya waathiriwa wa dhulma hizo, kati ya mwaka2011-12 walikuwa chini ya umri wa miaka 17 na takriban wote walibakwa.
Nchini Sierra Leone, baada ya vita, zaidi ya asilimia 70 ya unyanyasaji wa kingono ulifanyiwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 18, na zaidi ya nusu yao walikuwa chini ya umri wa miaka 11.
Katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, takriban thuluthi mbili ya visa vya ubakaji vilivyorekodiwa na UN mwaka
2008, vilihusisha watoto na wengi wao wakiwa wale waliovunja ungo.
Wasichana na wavulana wanatekwa nyara na kudhulumiwa na wanajeshi pamoja na makundi ya wapiganaji , kwa mujibu wa shirika hilo.
chanzo:bbcswahili
Ripoti hiyo inasema kuwa watoto huathirika kimaisha.
0 comments: