Chakula kinavyoharibikia sokoni Afrika
Soko la Marikiti ndilo lenye
idadi kubwa ya wauzaji wa mgoga na matunda. Chakula huletwa katika soko
hili kutoka kote nchini Kenya
Wanafunzi wa shule ya upili ya St
Georges nao pia walifika kwenye soko la Marikiti kujionea shughuli za
uuzaji na hata kuwa wauzaji kwa siku hiyo
Je unafahamu kiwango cha chakula ambacho huharibiwa sokoni na ambacho ikiwa kingefika kwa meza za watu, basi nchi nyingi Afrika zisingekuwa na njaa?
Amini usiamini jambo hili hufanyika katika masoko mngei barani Afrika mji wa Nairobi ukiwa haujaachwa nyuma.
Mwaka huu dunia ilipoadhimisha siku ya mazingira duniani, wasanii mashuhuri mjini Nairobi Kenya walijitokeza kuhamasisha wafanyabiashara sokoni nyenzo za kuzuia kuharibika kwa chakula kikiwa sokoni huku nao wakigeuka wafanyabiashara kwa siku hiyo.
M,pango wa umoja wa mataifa wa kulinda mazingira UNEP, ndio ulidhamini mradi huo maalum. Shirika hilo linasema kuwa karibu thuluthi moja ya chakula katika mataifa ya kiafrika kuharibiwa hata kabla ya kufika sokoni.
Emmanuel Igunza alishuhudia harakati za wasanii hao na kupiga picha hizi
chanzo:bbcswahili
0 comments: