Shambulizi kubwa dhidi ya UN Somalia
Watu waliokuwa wamejihami wameshambulia makao ya umoja wa mataifa mjini Mogadishu Somalia .
Mlipuko mkubwa ulisikika ukifuatiwa na milio mikubwa ya risasi.Makao yenyewe yako karibu na uwanja wa ndege na yana nyumba za wafanyakazi wa umoja wa mataifa .
Wavamizi walishambulia ofisi za makao ya shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu.
Majeshi ya Somalia na yale ya Muungano wa Afrika, walizingira makao ya shirika hilo na kuanza kufyatua risasi kujaribu kuwatimua washambuliaji hao.
Kiwango cha uharibifu bado hakijulikani. Ofisi hizo ni makao kwa maafisa wa Umoja wa mataifa walio mjini Mogadishu.Hili ndilo shambulizi kubwa zaidi kushuhudiwa kwa siku za karibuni dhidi ya Umoja wa mataifa mjini Mogadishu
chanzo:bbcswahili
0 comments: