HILI LAWEZA KUFUNGA MWAKA,SIKIA :MAKOSA ATANGAZA KUJINYONGA KWA KIINGILIO, ALIKUWA MFANYABIASHARA MAARUFU SANA MJINI IRINGA
Katika mazingira ya kutatanisha Makosa ametangaza kujinyonga katika
tukio atakalolifanya hadharani. Kwanini anataka kulifanya tukio hili
hadharani? Hili ni swali ambalo kila mtu anaweza kujiuliza lakini jibu
lake anataka iwe hivyo kwa kuwa atajinyonga katika tukio ambalo
mashuhuda watalazimika kulipa kiingilio. Kwanini anataka kufanya tukio
hilo kwa kiingilio? Kila mtu anaweza kujiuliza swali hili. Katika majibu
yake kupitia mtandao huu, MAKOSA anasema amefikia uamuzi huo ili
zikusanywe fedha zikazosaidia kuendesha familia yake, watoto yatima na
sehemu kuchonga madawati kwa shule zenye upungufu wa madawati mjini
Iringa. Alipoulizwa kama ana ufahamu wa sheria na kwamba kujaribu au
kufanya hivyo ni kosa la jinai, katika majibu yake anasema litakuwa kosa
la jinai mpaka pale atakapofanya hivyo na kwa kuwa atakufa hana cha
kuhofia. Lakini MAKOSA ni nani? Kwa wakazi wa mjini Iringa MAKOSA ni mtu
maarufu sana, alifahamika zaidi kwa biashara zake nyingi alizoanza
kuzifanya mwanzoni mwa miaka ya tisini baada ya kuacha shughuli yake ya
ubaharia. Wakati akifika mjini Iringa, MAKOSA akiwa na itikadi za rasta,
alikuwa hanywi pombe, mnyenyekevu na alijikita katika kuisaidia jamii
ya watu wa Iringa kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti. Miti ya aina
mbalimbali inayonekana mjini Iringa, sehemu yake kubwa ilipandwa na
MAKOSA. Hata hivyo pamoja na kuupendezesha mji kwa miti hiyo, historia
ya MAKOSA katika uhifadhi wa mazingira ni kama vile imesahaulika
kwasababu hakuna anayemuenzi kwa kazi kubwa aliyoifanya. Pamoja na
harakati hizo MAKOSA ndio mtu wa kwanza mjini Iringa kuingiza magari
aina ya Coaster zilizokuwa zikifanya kazi ya kusafirisha abiria katika
maeneo mbalimbali ya mjini Iringa. Pamoja na biashara ya usafirishaji,
MAKOSA alikuwa anaendesha biashara ya hoteli. Kabla ya kuanza kuendeshwa
na MAKOSA, hoteli hiyo ilikuwa ikijulikana Cats Hotel (ipo jirani na
Maktaba ya Mkoa wa Iringa) na akaibadilisha jina na kuiita MAKOSA CATS
Hotel. Katika hoteli hiyo bendi nyingi zimepiga muziki na kwa mara ya
mwisho, mwanamuziki Macay Fanta alikuwa akifanya shoo zake mpaka pale
MAKOSA aliposhindwa kuiendesha mwanzoni mwa miaka ya 2000. Lakini
mtandao wa biashara za makosa haukuishia hapo, alikuwa pia akimiliki
hospitali maarufu sana iliyopo jirani kabisa na soko kuu la mjini
Iringa, hii nayo iliitwa MAKOSA hospital. Taarifa kutoka kwake mwenyewe
biashara zote hizo haziko tena mikononi mwake na ugumu wa maisha unazidi
kumuandama. Japokuwa hajasema hivyo, huenda kuteteleka kwa hayo yote
ndio sababu ya MAKOSA kutaka kujiua. Tafsiri ya jina la MAKOSA
imeendelea kuwa siri yake na amekataa kutoa maana ya kuacha majina yake
halisi ya Ramadhani Mrisho na kujiita MAKOSA.
Chanzo: Frankleonard blog

0 comments: