MTUHUMIWA WA UGAIDI WA MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA KANISANI JIJINI ARUSHA AKABIDHIWA HATI YA MSHTAKA...!!
Ambrose
Hakimu
wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Devotha Kamuzora jana alimkabidhi
hati ya mashitaka yanayomkabili, Victor Ambrose (20) ambaye ni mtuhumiwa
pekee aliyepandishwa kizimbani baada ya kutokea shambulio la bomu
katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti jijini Arusha.
Ambrose alikabidhiwa hati hiyo ya mashitaka yanayomkabili jana katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru jijini Arusha na kuambiwa na wakili wa Serikali, Adelaide Kasala kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo, haujakamilika na kumuomba Hakimu Kamuzora kutaja tarehe nyingine.
Hakimu Kamuzora kabla ya kuahirisha kesi hiyo alimuuliza Ambrose kama alipewa hati yake dhidi ya mshitaka yanayomkabili. Ambrose alipojibu, “hapana.” Baada ya jibu hilo,
Ambrose ambaye ni dereva wa bodaboda na mkazi wa Mrombo jijini Arusha, mara ya kwanza alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Arusha na baadaye kuhamishiwa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru na kusomewa mashitaka yake kwa mara ya tatu sasa huku akitakiwa kutojibu lolote, kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji.
Wakili wa Serikali, Adelaide Kasala alidai mahakamani hapo Victor alitenda makosa hayo Mei 5, mwaka huu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti jijini.

Hakimu alitoa hati hiyo na Ambrose kukabidhiwa na kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 24.

0 comments: