Besigye apinga matokeo ya uchaguzi Uganda
Mmoja wa wapinzani wakuu katika
uchaguzi mkuu uliomalizika hivi punde nchini Uganda, Dkt Kizza Besigye,
amekatalia mbali matokeo ya uchaguzi huo, uliofanyika siku ya Alhamisi.
Bw
Besigye ambaye amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake tangu siku ya Ijumaa
amesema kuwa raia nchini Uganda wameshuhudia ulaghai mkubwa mno wa
uchaguzi mkuu, kuwahi kufanyika katika taifa hilo la mashariki mwa
Afrika.Kanali huyo mstaafu ameelezea uchaguzi huo kama usio halali na kuwa ni mapinduzi ya kijeshi.
Rais wa muda mrefu Yoweri Kaguta Museveni, alitangazwa mshindi.
ZAIDI BOFYA HAPA CHINI:
http://www.bbc.com

0 comments: