Mwandishi wa Habari Burundi akamatwa.
Viongozi nchini Burundi wamethibitisha kukamatwa kwa mmoja wa watangazaji wa Televisheni moja nchini humo pamoja na watu wengine watatu siku ya Alhamis.
Msemaji wa Idara ya usalama wa taifa ya Burundi, Telesphore Bigirimana amesema mwandishi huyo Lucien Rukevya hajawahi kushitakiwa kwa makosa yoyote ya jinai lakini anashikiliwa kwa kuvunja sheria za usalama wa nchi.Msemaji huyo aliendelea kwa kusema watu wengine watatu wanaoshikiliwa ni ni waziri wa zamani Ignace Bankamwabo na watu wengine wawili raia wa Congo ambao wanadhaniwa kuwahi kuwa wapiganaji wa Kundi la M23 la Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo.
Chama cha waandishi wa habari nchini Burundi kimesema bwana Rukevya ni mwandishi wa tatu nchini humo kukamatwa tangu kupitishwa kwa sheria mpya yenye utata mwanzoni mwa mwezi huu.
chanzo:bbc swahili
0 comments: