Polisi waondoka medani ya Taksim
Baada ya mapambano ya siku mbili
na waandamanaji, polisi wameondoka katika medani ya Taksim mjini
Istanbul na maelfu ya waandamanaji wameikalia medani hiyo.
Lakini Bwana Erdogan ameahidi kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba polisi walitumia nguvu nyingi.
Nchi kadha zimeeleza wasiwasi kuhusu swala hilo.
Chanzo cha maandamano ni mpango wa kujenga maduka katika medani ya Taksim - mpango ambao Bwana Erdogan anasema atautekeleza.
Waandamanaji vijana piya wanailaumu serikali kwamba imekuwa ya kimabavu na kuifanya nchi kufuata Uislamu.
Msemaji wa serikali alikanusha malalamiko hayo alipohojiwa na BBC na alisema tuhuma zenyewe ni za kushangaza
Na bbcswahili
0 comments: