Waziri mkuu wa China atambelea Berlin
Ziara ya waziri mkuu wa China mjini Berlin, mtego wa ndege zisizokuwa na
rubani, kampeni ya uchaguzi mkuu na fainali ya kombe la vilabu bingwa
barani Ulaya Champions League ndizo mada zilizohanikiza magazetini.
Tuanzie lakini Berlin na ziara ya waziri mkuu wa jamhuri ya umma wa
China Li Keqiang. Umoja wa Ulaya unaikosoa China miongoni mwa mengineyo
kuhusu bei ya chini kabisa ya mitambo ya kunasia nguvu za jua. Hata
hivyo gazeti la "Stuttgarter Zeitung" linaandika:Kansela Angela Merkel
anataka kujitahidi kuuepusha mvutano huo usizidi makali.Kansela Merkel
sawa na waziri wa uchumi Philipp Rösler ameelezea nia ya kusaka
maridhiano ambayo ni kwa masilahi ya Ujerumani. China sio tu inazidi
kujipatia umuhimu barani Ulaya kwasababu ya matatizo ya kiuchumi katika
nchi nyingi za kanda ya Euro bali pia akiba kubwa ya sarafu ya nchi hiyo
tajiri inazifanya nchi za kanda ya Euro zisifanye mchezo. Hata hivyo
hiyo isiwe sababu ya kutozungumziwa masuala yanayozusha mivutano. Umoja
wa Ulaya una kila sababu ya kukosoa mtindo wa kibiashara wa China. Na
miaka ya nyuma imedhihirisha pia uwezekano upo wa kuepusha mvutano
usizidi makali.
Dw swahili
0 comments: