kama Kenya imewezekana kwanini Tanzania isiwezekane?
Wafungwa kuwaakilisha wenzao mahakamani-Kenya
Mmoja wa wafungwa katika jela la Shimo la Tewa mjini Mombasa, Douglas Owiyo, ameiambia BBC kuwa wao walaifanikiwa kumsaidia moja wao ambaye alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha na badala yake kufungwa miaka saba pekee.
Vile vile wafungwa hao walifanikiwa kumshauri mfungwa mwingine kukata rufaa na sasa ameachiliwa huru.
Tangu mwaka wa 2007, wakati Owiyo na wafungwa wengine walipoanza kufunzwa masuala ya sheria, tayari wamewasilisha mahakamani zaidi ya rufaa elfu tatu ambazo zimefanikiwa, licha ya kuwa wao sio mawakili waliohitimu.
Nchini Kenya, idadi kubwa ya watu wanaofikishwa mahakamani kwa mashtaka kadhaa huwa hawana mawakili wa kuwatetea.
Alipofikishwa mbele ya hakimu, kwa madai ya kuhusika na wizi wa mabavu, hakuwa na ufahamu wa kujibu mashtaka au jinsi ya kujitetea.
Kwa mujibu wa sheria za Kenya, mtu akipatikana na hatia ya kuhusika na wizi wa mabavu huhukumiwa kifo, na kabla ya kufahamu yale yaliyokuwa mbele yake, tayari alikuwa anakabiliwa na adhabu ya kifo.
Wafungwa kuwateteza wenzao mahakamani
Owiyo pamoja na wafungwa wengine ambao wamejifunza sheria, walianzisha mikakati ya kuandika nyaraka ambazo Moka atawasilisha wakati wa kukata rufaa.Amini usiamini rufaa yao ilikubalika na mahama.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo alikubaliana na wafungwa hao kuwa Moka hakustahili kufunguliwa mashtaka ya wizi wa mabavu na badala yake anastahili adhabu ndogo.
'' Wakati nilihukumiwa kifo, nilidhani nitarukwa na akili'' Alisema Moka.
''Lakini kwa ushauri wa wafungwa wenzangu ambao ni wasomi wa masuala ya sheria, nina matumaini tena'' Aliongeza Moka.
'' Visa kama hivyo ni vingi, kwa mfano, mtu anaweza kufunguliwa mashtaka ya kupatikana na silaha kwa nia ya kuiba, na akiri ndiyo alipatikana na silaha''
''Hapa jambo kuu ni kuwa hakuwa na nia ya kuiba. Ikiwa angelifahamu masuala ya kimsingi kuhusu sheria, hangelikiri kumiliki silaha''.
Hakimu huyo amesema, matokeo ya wafungwa hao kufundishwa masuala ya sheria, imeanza kujitokeza wakati wafungwa ao wanapofikishwa mahakamani.
''Punde to wanapo shauriwa na wataalamu hao wa kisheria wanafahamu haki zao'' Alisema hakimu huyo.
Wafungwa sasa wanauliza nyaraka za mashahizi, na mara nyingine huomba kesi kuhairishwa ili waandae tetesi zao.
Hakimu huyo wa Mombasa ameongeza kusema kuwa baadhi ya wafungwa hao hata kuwasilisha hoja za kisheria.
Shirika linalohusika na mpango huo wa kutoa mafunzo ya sheria kwa wafungwa ni Kituo cha Sheria.
Kituo hicho kiliundwa kwa wa 1973, na kundi la mawakili ambao walikuwa na nia ya kuwapa usaidizi washitakiwa ambao mara nyingi hawana uwezo wa kuwa na mawakili.
Kwa sasa shirika hilo la Kituo cha Sheria kimeimarisha huduma zake na mbali na kutoa mafunzo wa wafungwa pia ni miongoni mwa makundi yanayotetea haki za kibinadam na utawala bora nchini Kenya.
Shirika hilo inahusika na kampeini ya kushinikiza serikali kufutilia mbali adhabu ya kifo nchini Kenya, licha ya kuwa hakuna mfungwa ambaye amewahi kunyongwa tangu mwaka wa 1987.
Kufuatia ufanisi huo katika jela la Shimo la Tewa Mjini Mombasa shirika hilo la Kituo cha Sheria kwa sasa linaendesha mafunzo kama hayo katika jela lenye ulinzi mkali la Kamiti na lile la kina mama la Langata mjini Nairobi.
Joseph Karanja ambaye ni mkuu wa idara hiyo katika jela la Kamiti amesema katika kipindi cha miezi tisa tangu kuanzishwa kwa mafunzo hayo, wameshinda kesi mia moja ishirini.
Takwimu hizo zimethibitishwa na afisa mkuu anayesimamia jela hilo la Kamiri Senior Sergeant Benson Ngui, ambaye anasema kabla ya mafunzo hayo kuanzishwa alitarajia rufaa chache kupita mwaka mmoja.
Basi imekuaje mawakili hao wafungwa wakaweza kushinda kesi nyingi hivi?
Wanasema kuwa walitumia mipenyo katika sheria na kudhihirisha uzembe kutoka upande wa mashtaka na uchunguzi mbovu wa idara ya polisi na uamuzi wa kiholela kutoka kwa majaji."Tunajaribu kuonyesha kuwa kesi haikufanyika kwa njia salama. Kwa mfano katika kesi ya unyanyasaji wa kimapenzi wa mtoto wa chini ya umri, ambapo mhasiriwa hakuwahi fanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na ushahidi umetegemea zaidi taarifa kutoka kwa mazazi wa mtoto, ambaye huenda akawa na kisasi na mshukiwa,'' asema, Denga John Lenda, naibu mkuu wa wanafunzi wa sheria katika jela la Kamiti.
Karanja, anajivunia kuwa, hata wale wafungwa ambao tayari wana mawakili wao wanaamua kuwaacha na kutafuta usaidizi wa kisheria kutoka kwa wafungwa wenzao.
Kwa mujibu wa katiba ya Kenya, mwananchi yeyote anayo haki ya kupata uakilishi wa kisheria kwa ufadhili wa serikali ''iwapo kuna hofu ya haki kuvunjwa''.
Allan Nyange, ambaye ni mwanasheria katika shirika lisilo la kiserikali la Kituo cha Sheria anaeleza kuwa wakati mwingine hao mawakili wa kukodiwa huwa kizuizi kikubwa katika kesi badala ya usaidizi.
"Hebu fikiria, mara nyingi ni kesi inayolazimishwa kwa wakili huyo, yeye hana haja na masuala ya uhalifu. Analenga mengine makubwa yaliyo na malipo ya juu zaidi na anachukulia hili kama suala la kumpotezea muda wake.'' Anaeleza Allan.
"Kwa hivyo mara nyingi unakuta mawakili kama hao hawajisumbui na kesi wanazopewa, wanafanya juhudi zote kutafuta kuahirishwa kwa kesi.''
kwa Bwana Nyange hakuna shaka yoyote kwa ufanisi wa mawakili hao wafungwa.
"Nakuhakikishia kuwa wengi wao ni bora kuwaliko wale mawakili wa nje. Wale waliopewa mafunzo.'' Anasema.
"wao wako na muda wa ziada. Na wanapata msukumo kutokana na kuwa wanaweza kupiga chenga mfumo uliopo kupitia sheria na ukifaulu unaweza kwenda nyumbani.''
Lakini nini kinafanyika baada ya hawa mawakili wafungwa kutoka jela?
Baada ya kukaa zaidi ya miaka 13 akisubiri kunyongwa, hatimaye alishinda rufaa yake na akaachiliwa mwaka wa 2010.
Yeye anasifiwa kwamba amewasaidia zaidi ya wafungwa 250 kuachiliwa huru kutokana na uakilishi wake.
Lakini tangu kuachiliwa kwake, amekuwa akifanya kazi katika mahakama za Mombasa, ila sio kwa njia inayotumia ujuzi wake wa sheria, anafanya kazi ya kusafisha vyoo katika mahakama hiyo. Anasema kuwa ni huu ndio wito wake.
Hatma ya mawakili?
Bwana Omondi anahitaji kupata pesa za matumizi na kwa sasa wanafunzi wa sheria kama yeye hawaruhusiwi kulipisha wateja wao kwa huduma wanayotoa.Licha ya ufanisi huo wa mawakili wafungwa, baadhi ya wamakili waliohitimu wameelezea wasi wao kuwa kundi hili la mawakili linaweza kuwahadaa wanainchi.
Lakini mawakili hao wafungwa wamepata mshirika wa karibu Jaji mkuu wa Kenya Willy Mutunga.
Mutunga ni mmoja wa mawakili waliopigania sana haki za kibinadam nchini Kenya na pia mmoja wa waanzilishi wa shirika la Kituo cha Sheria.
''Kutokana na kile ambacho nimeona kutoka kwa mawakili hao wafungwa, sina shaka kuwa wanaweza kufan ya kazi nzuri'' Alisema Jaji Mutunga.
''Ikiwa unazungumza kuhusu haki, na mtu aje mahakamani na kusema sina wakili lakini nina wakili huyu mfungwa kuniakilisha, ni sharti ikubalike kama jambo sahihi aliongeza Mutunga.
Jaji Mutunga amesema ni sharti watafute mbinu za kuwashirikisha mawakili hao wafungwa katika mfumo wa mahakama.
''Chama cha wanasheria nchini Kenya, LSK ni sharti iidhinishe mawakili hao wafungwa kama njia moja ya kuharakisha utoaji wa haki katika mahakama'' Aliongeza Mutunga.
0 comments: