Safari ya kupata elimu:kwa Tanzania ni kazi kwelikweli(noma)

...................
Sylvia na Mamake nje ya nyumba yao

Sylvia ni msichana wa miaka minane anaishi kijiji kimoja Tanzania, licha ya maisha yake amejitolea kupata elimu na kila siku hutembea kwa saa moja unusu kwenda shuleni. Yeye ni miongoni mwa wasichana waliobahatika kupata elimu Barani Afrika
Sylvia akielekea shuleni anapitia njia tofauti

Mtoto huyu hupitia njia nyingi familia yake ni masikini na haiwezi kumnunulia viatu. Japo hakuna karo anayolipiwa, imekua vigumu kwa wazazi wake kununua vitabu au sare za Sylvia za shule.

Lori hili lampita Sylvia akielekea shuleni

Safari ya msichana huyu kisha inampeleka barabara kuu. Wakati mwingine kuna jua kali, vumbi nyingi. Msimu wa jua barabara hujaa mapote na inampa changamoto msichana huyu katika safari yake shuleni

Sylvia akitumia njia ya reli kuelekea shuleni

Ikiwa msichana huyu hataki vumbi na matope ya barabara, huamua kupitia kwenye njia ya reli. Hata hivyo kuna hatari zake, treni huenda ikaamkanyanga. Wakati mwingine watoto wa shule wamekua wakitekwa nyara.
Sylvia akipitia  kichochoro kueleka shuleni

Kuna vichochoro vingine kando ya barabara kuu ambavyo Sylvia hutumia, lakini kuna hatari ya kukumbana na wabakaji.

Sylvia akielekea kuingia shuleni

Baada ya pita pita hizo hatimae Sylvia huwasili shuleni.Msichana huyu anasema ataendelea na elimu yake licha ya safari ndefu ambayo hufanya kila siku.

Sylvia anaelekea darasani

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na Utawaduni-UNESCO asili mia 62 ya wasichana Afrika wameweza kuingia shule za upili, hata hivyo nchini Tanzania ni asili mia 32 pekee ya wasichana ambao wanaweza kujiunga na shule za upili.

  11 Julai, 2013 - Saa 10:34 GMT
Sylvia na familia yake
Sylvia na familia yake
Baba wa kambo wa Sylvia amekua akiona malezi yake kama mzigo hasa elimu, lakini kwake Sylvia anasema elimu ni njia pekee ya kubadilisha maisha ya familia yake


chanzo:bbcswahili.
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: