TZ yawaaga wanajeshi waliouawa Darfur
Rais wa Tanzania Jakaya Kiwete
amewaongoza maelfu ya waombolezaji katika kutoa heshima zao za mwisho
kwa wanajeshi saba wa Tanzania waliouawa nchini Sudan.
Saba hao walikuwa katika harakati za kulinda
amani chini ya Muungano wa Afrika katika jimbo la Darfur nchini Sudan
tarehe 13 mwezi Julai.Hafla ya kuwaaga wanajeshi hao inaendelea katika uwanja wa makao makuu ya jeshi eneo la Upanga.
Rais Kikwete anawaongoza jamaa familia na rafiki wa wanajeshi hao kuwapa heshima zao za mwisho kabla ya maziko nyumbani kwao.
Wanajeshi hao wa TPDF ni pamoja na Sajenti Shaibu Shehe, Corporal Oswald Chaulo, Corporal Mohammed Ally, Corporal Mohammed Chukilizo, Private Rodney Ndunguru, Private Fortunatus Msofe na Private Peter Werema.
Rais wa Sudan Omar Al Bashir wiki jana alimhakikishia rais Jakaya Kikwete kuwa wote waliohusika katika kuwashambulia wanajeshi hao na kuwaua watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Rais Bashir alitoa ahadi hiyo wakati wa mazungumzo na Kikwete akiongeza kuwa anaamini waliohusika na mauaji hayo walikuwa wahalifu na kuwa lazima wasakwe.
chanzo:bbcswahili
0 comments: