Zuma amfuta kazi mpiganiaji wa Uhuru
Tokyo Sexwale
Rais Jacob Zuma, wa Afrika
Kusini, amemfuta kazi waziri wake wa nyumba na mkereketwa na vita dhidi
ya ubaguzi wa rangi nchini humo Tokyo Sexwale.
Bwana Sexwale ni mmoja wa mawazirei ambao
watapoteza nyadhifa zao katika kile rais Zuma, alichokitaja kama mpango
wa kuimarisha huduma za serikali.Wachanganusi wa masuala ya kisiasa hata hivyo wanasema kuwa Bwana Sexwale amefutwa kwa kuwa alihusika na kampeini ya kumuondoa rais Zuma mwaka uliopita.
Sexwale alifungwa katika gereza la Robben Island pamoja na rais wa kwanza wa nchi hiyo Nelson Mandela.
Yeye ni pia afisa wa ngazi ya juu wa shirikisho la mchezo wa soka duniani Fifa.
chanzo:bbcswahili

0 comments: