MUME WA MTU KAMA UNATABIA HII ACHA
mume wa mtu afumwa guest na mke wa mtu mkewe awa shuhuda wakati wa fumanizi
SHETANI
anazidi kuiatamia dunia, ulimwengu unawayawaya! Jamaa mmoja aliyetajwa
kwa jina moja la Manfree, mkazi wa Kimara Mwisho, Dar ambaye inadaiwa ni
mfanyabiashara wa baa iliyopo Mbezi Mwisho (Mbezi Shamba) anadaiwa
kunaswa na mke wa mtu (jina tunalo), Risasi Mchanganyiko linaibumburua.
Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lililoongeza faraja na furaha ya shetani kule kuzimu, lilijiri juzikati huko Kimara Mwisho ndani ya gesti moja (jina lipo kwenye droo zetu).
ALIYENASA AANZA KUMWAGIKA
Akizungumza kwa uchungu mkubwa, mume wa mwanamke huyo ambaye hakupenda jina lake liupambe ukurasa huu, alisema siku nyingi Manfree amekuwa akimsumbua mke wake, hali iliyokuwa ikimpa wakati mgumu mwanamme huyo mwenye mke.
“Jamaa amekuwa akimsumbua sana mke wangu, nilipokuja kuzipata taarifa hizi nilishangaa sana lakini pia niliumia kama mwanamme,” alisema mwenye mke huyo.
MAZOEA YALIPOANZA
Kwa mujibu wa mume huyo, kufahamiana kwa Manfree na mkewe kulikolea zaidi baada ya mwanamke huyo kuhitaji fremu kwa ajili ya biashara ya duka ambapo kwa kutumia uenyeji wa jamaa huyo, alionesha kutaka kumsaidia.
SINEMA YA KUNASWA ILIPOANZA
Mwanamme huyo aliendelea kusema kuwa sinema ya kunaswa kwa mwanamme huyo ilianza siku moja baada ya yeye kwenda kwenye baa ya jamaa huyo kuangalia mpira (hakuzitaja timu).Alisema akiwa hapo baa, mara mke wake alitokea na kukaa kwenye kiti, meza nyingine. Jamaa huyo naye akaenda kukaa na mke wa jamaa na kuanza kuzungumza.
“Mimi sikujua walichokuwa wakikizungumza na wala sikuwa na wasiwasi kwa vile jamaa ananifahamu, anafahamu yule ni mke wangu na anawafahamu hadi watoto wangu,” alisema mwanamme huyo.Akaongeza: “Tulipofika nyumbani, mke wangu akasema amesikia mimi nina wanawake wengi nje, nimewafungulia biashara na mambo mengine kibao.
“Nilimuuliza ameambiwa na nani, akawa anagomagoma kunijibu lakini nilipombana sana mwisho akamtaja jamaa. Kumbe alipokaa naye pale baa ndiyo alikuwa akimwambia uongo huo.“Mke wangu akaongeza kusema kuwa jamaa huyo kwa muda mrefu amekuwa akimtaka wakutane ‘praiveti’ lakini yeye amekuwa akimkatalia kwa sababu analinda heshima ya ndoa yake.
“Mke wangu alinionesha meseji ambazo jamaa alikuwa akimtumia, niliumia sana. Kwa kweli inauma sana jamani hasa kitendo hicho kufanywa na mtu ambaye mnafahamiana!”
CREDIT TO SHADDY
0 comments: