UMEIPATA HII.. REFA APEWA KADI NYEKUNDU
Mchezaji amwonesha refa kadi nyekundu Uturuki
Mchezaji wa klabu
ya Trabzonspor, Salih Dursun, alitolewa nje kwa kumuonyesha mwamuzi kadi
nyekundu wakati wa mchezo waliofungwa mabao 2-1 na Galatasaray katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki.
Tukio hilo lilitokea dakika ya 86
ya mchezo, klabu hizo zikiwa zimetoshana nguvu 1-1, baada ya mwamuzi
Denis Bitnel kumuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Luis Cavanda kwa
kufanya madhambi ndani ya eneo la hatari. Aidha, aliwazawadi
Galatasaray penalti.
Trabzonspor walikuwa tayari wamesalia wachezaji tisa uwanjani kabla ya kutokea kwa kisa hicho.
Wachezaji wa Trabzospor walimzingira mwamuzi kupinga kadi hiyo.
Ni
wakati huo ambapo Dursun alimnyang’anya refa kadi nyekundu aliyokuwa
nayo na kumuonyesha kadi hiyo hatua ambayo ilipelekea na yeye kufukuzwa
uwanjani.
chanzo:bbcswahili

0 comments: